Posts

Showing posts from May, 2017

TUTAWAGUNDUA WOTE WANAOINGIZA DAWA ZA KULEVYA ZANZIBAR

Image
Na mwandishi wetu. Licha ya serikali kupambana vikali  na tatizo la  uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya lakini bado tatizo hilo linaendelea kuwa endelevu katika  maeneo mengi  nchini tanzania. Akiongea na mwandishi wetu huko ofisi ya wilaya ya kusini unguja Dr IDRISA MUSLIM HIJJA amefahamisha kuwa kwa wale wanaojinufaisha kwa kuathiri wengine amboa kundi lengwa la wapenda kuiga mambo yasiyo na faida kwao, Dr Idrisa amesema ijulikane kuwa waathirika wakuu wa dawa hizo ni vijana na ndio nguvukazi na tegemeo la taifa lololte katika kulipa maendeleo.       Hivyo wakati umefika kwa vijanao kuijua thamani yao kwa kuachana na vitendo hivo  ili kwa usalama wa afya zao na maendeleo ya taifa. hata hivyo mkuu wa mkoa huyo DR. IDRISA MUSLIM HIJJA wakati akizungumzia mikakati na hatua walizochukua  kwa wale wote wanaojihusisha na uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya huko ofisi ya wilaya  ya kusini  ilioko makundundichi mkoa wa kusini unguja. Amesema tayari ameshape

UMWAGAJI TAKA OVYO MITAANI NI CHACHU YA KUENEZA MARADHI YA MIRIPUKO

Image
Na mwandishi wetu Katika kuweka hali bora ya afya  wananchi wanatakiwa  kuwa  wepesi katika kumwaga taka kwenye makontena ili kuepusha uzagaaji wa taka ovyo hali inayosababisha kutokea kwa maradhi mbali  mbali ikiwemo ya miripuko. Pia  akina mama majumbani  na wafanya biashara  wanatakiwa kuwatuma watu wenye ufahamu pindi wanapokwenda kumwaga taka kwa usalama wa afya zao  na wataifa kwa ujumla. Wito huo umetolewa na Afisa Mahusiano wa Baraza la Manispaa Zanzibar  Haitham Mzee Yussuf wakati akizungumza na mwandishi wetu huku ofisini kwake malindi mjini unguja amewataka wananchi kuwa wepesi wa kumwaga taka ili kuepusha mrundikano wa takataka na kutupwa taka hizo na watu wenye uwelewa wa utupaji wa taka ili kuepusha kumwaga nje ya makontena au pahala ambapo haparuhusiwi kisheria hususan kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini   Hata hivyo akaitaka jamii kuwa waangalifu wa utunzaji na utumiaji wa maji na vyakula kwani kuna taarifa za kuanza kupatikana wago

MASJID MTAMBANI YATOA TAMKO KUHUSU MAUWAJI YA KIHOLELA NA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA ZA MOTO NCHINI TANZANIA

Image
MASJID MTAMBANI YATOA TAMKO KUHUSU MAUAJI YA KIHOLELA NA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA ZA MOTO. Na  Mwl Razaq Mtele Malilo  jijini dar es salaam Masjid Mtambani ni Msikiti uliopo maeneo ya Kinondoni Jiji Dar Es Salaam leo kupitia Imamu wa Msikiti huo umetoa tamko zito kuhusu hali ya usalama nchi hususani matumizi holela ya silaha za moto na mauaji ya mara Kwa mara ya raia na jeshi la polisi. Imamu wa Mtambani akiwahutubia waumini waliokuwa wamehudhuria kuswali ibada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti huo wa Mtambani Leo Mei 19/2017 katika hotuba yake iliyohusu kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini pia katika hotuba yake ya pili aligusia masuala ya matumizi mabaya ya silaha za moto na mauji ya raia wasio na hatia na mauwaji ya jeshi la polisi. Katika matumizi mabaya ya silaha za moto  Imamu aligusia kutishiwa bastora Kwa aliyekuwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe Nape Nnauye na kitendo cha Polisi kupiga risasi hewani kwenye tukio la aliyekuwa naibu waziri wa

ZANZIBAR CLIMATE CHANGE YAWAANDAA WANAHABARI KUWA MABALOZI WA MAZINGIRA ZANZIBAR

Na Ali Abdalla Ayoub (Bin Ghullam) Zanzibar climate change wameandaa mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wa wanahabari ili kuibua maeneo muhimu ya utoaji elimu na utetezi kuhusiana na uhifadhi wa mazingira na kukabiliana,kulindana kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi Zanzibar Akiongea wakati wa utoaji elimu kwa wanahabari SOUD MOHAMMED JUMA kwenye ofisi za taasisi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi Zanzibar ZACCA iliyopo mwanakwerekwe C  wilaya ya magharibi B Unguja amesema maeneo ambayo wameyaangalia zaidi ni pamoja na misitu,nishati,uvuvi,habari,miundombinu na maji  SOUD amesema kwa nchi za visiwa athari ni kubwa kutokana na kuchukuwa muda mrefu kurejesha hali halisi ya maeneo yanayokumbwa na athari za tabia nchi huku akipigi mfano uharibifu wa miundo mbinu kisiwani PEMBA na kimbunga kilicho ikimba Zanzibar juzi mpaka leo imeshindikana kuweza kuweka sawa maeneo yaliyo athirika. Akizungumzia suala la athari za mchanga ambao ulikuwa

KUNYESHA KWA NVUA KWENYE VISIWA VYA ZANZIBAR YAWA ADHABU KWA WAKAAZI WA KINUNI

Image
Na mwandishi wetu Kufuatia nvua zinazoendelea kunyesha kote nchini na kusababisha maeneo kadhaa kujaa maji ikiwa ni pamoja na miundo mbinu ya bara bara kuharibika vibaya na kusababisha usafiri kuwa mgumu wa DALADALA na kupelekea wakaazi wa kinuni kulazimika kulipia nauli ya shilingi mia tano (500) tofauti na nauli ya kawaida ya shilingi mianne (400)    Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwa huzuni kwenye daladala hizo abiria ambao ni wakaazi wa eneo la kinuni wamekuwa wakihoji juu ya mamlaka zinazohusika na miundombinu kuwasahau jambo linalowapa wasiwasi kuwa wamesahaulika katika taifa lao    Kwa upande wao makondakta na madereva wa daladala hizo wamedai kuwa tayari wameshapeleka malalamiko yao juu ya ubovu wa bara bara hiyo ambo inaongoza njia za ndani kwa idadi kubwa ya abiria.   Wamesema wao wanalipia stahiki zote za njia lakini kinacha washangaza bara bara hiyo ikiharibika wakati wa nvua hulazimika kujaza kifusi ili kupata sehemu ya kupitisha gari zao, baada ya kumaliza kuj

HALI ILIVYO KWENYE JIMBO LA CHAKE CHAKE KUJAA MAJI KWA MSIKITI WA AFRIKANA

Image
KUJAA MAJI KWA MSIKITI WA AFRIKANA NI MAKOSA YA WAJENZI. Ameandika SAIDI MIRAJI ABDALLA katika ukurasa wake wa FACEBOOK kuwa "Kwa mimi niliezaliwa na kukulia katika mji wa Chake Chake Pemba na ninae vijua vyema viunga vya mji huo, hainishangazi kamwe kwa eneo lililojengwa msikiti huu hapo Miembeni maarufu Afrikana kujaa maji kihivi. Wajenzi wa msikiti huu walipaswa kujua historia ya mahali walipotumia mamilioni ya fedha na jografia yake ili wajue namna ya ujenzi u liopaswa kujengwa mahali hapo". Pembezoni mwa msikiti huo kuna mto unaopokea maji kutoka sehemu za vitongoji, kupitia wawi, machomanne, michakaeni, shamiani, mtoni, msingini na kuyapeleka, bandataka hadi nkokota ngozi ambapo yana mwagika baharini, huko nyuma yanakotiririka maji hayo kutoka milimani husomba vitu vingi mvua zikiwa kubwa kidogo mto hujaa maji na kufurika, sababu njia yake ni nyembamba na una mchanga mwingi, hadi watu hutoa mchanga wa kujengea katika mto huo. Tatizo jengine ni kwamba baada ya mto huo kw

MBUNGE WA CHAKE CHAKE YUSUF KAIZA (CUF) ALIA NA MAAFA JIMBONI KWAKE

Image
 YUSUF KAIZA ALIA NA MAAFA JIMBONI KWAKE Akiongea na mwandishi wetu mbunge huyo wa jimbo la chake chake YUSUF KAIZA MAKAME  amesema "Nimeskia na nimeona, baadhi ya maafa yanayoendelea kutokea kutokana na mvua zinanazoendelea kunyesha Zanzibar hasa kwenye jimbo langu LA Chake - Chake. amesema amepokea simu kadhaa na pia ameona kwenye social media kuwa wadi ya Kibirinzi hasa maeneo ya Muharitani, Msingini, Mtoni na mengine ni maeneo yenye athari kwenye mvua zinazoendelea kunyesha". amesema kwa masikitiko makubwa kaiza pia amese "Pamoja na maeneo hayo, naamini mvua zinazoendelea kunyesha, zimeleta athari kwenye maeneo mengi ya watu wangu wa Chake - Chake. Athari  kubwa zaidi naamini ni za kijamii na kiuchumi". akionesha hisia zake KAIZA ametaja janga hilo katika sehemu kuu mbili ambapo  1.Kijamii: wapo wanaokosa makaazi/malazi, aidha nyumba zimeanguka ama zinavujisha hasa ktk maeneo ya Muharitani na Msingini. Pia nimeona, nyumba za ibada (Miskiti) zimejaa m

ZANZIBAR YATANGAZA SILAHA ZA MAANGAMIZI RIADHA

Image
ZANZIBAR YATANGAZA SILAHA ZA MAANGAMIZI RIADHA NA BIN GHULLAM   Kufuatia mashinda ya riadha ya afrika ya mashariki na kati yanayotarajiwa kufanyika jijini dar es  salaam chama cha riadha zanzibar kimetangaza wachezaji watakao iwakilisha zanzibar katika mashindano hayo mashindano  ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 13/14.05.2017 katika uwanja wa taifa jijini dar  kwa vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao kwa Zanzibar  itawakilishwa na Rosemary Gustafu  Kazija  ZainaAli Othmani HASSAN NSIMAI ASMA AYUBU YUSSUF  Omari Bakari ali, Abdullatif Murtaza Omar Bashir amesema Suleimani Ame Nyambui katibu wa riadha Zanzibar.  pia akitaja viongozi ambao wataambatana na wachezaji hao katiksa kuiwakilsha Zanzibar katika mashindano hayo ya Afrika mashariki na kati ni katibu Suleiman Nyambui, mwenyekiti Abdulhakim Cosmas na makamo mwenyekiti Mbarouk meneja wa timu muhidini yasin  vile vile timu hio itaongozana na waamuzi watakaoshirikiana na wenzao katik mashinda

"WANAHABARI WAFUATENI MAWAZIRI WAKUPENI TAARIFA " MAKAMU WA PILI WA RAISI BALOZI SEIF ALI IDDI

Image
WANAHABARI KUWENI HURU KUIYELIMISHA JAMII NJOONI OFISINI KWANGU Makamo wa pili wa raisi wa serikali ya mapinduzi ya ZANZIBAR mh BALOZI SEIF ALI IDDI amewataka wanahabari kuwa huru kuandika habari zenye kujenga jamii imara bila kujali vikwazo ambavyo vinawakuta na kitaja kama changamoto za kuwajenga katika taaluma yao    Katika maadhimisho hayo ya siku ya wanahabari duniani yaliyofanyika leo 03/05/2017 kwenye holi la chuo cha uwandishi wa habari kilimani mjini unguja BALOZI SEIF amesema raisi wa Zanzibar ambae pia ni mwenyekiti wa BARAZA la MAPINDUZI DR ALI MOHAMMED SHEIN amewataka mawaziri wote kutoa taarifa kwa wanahabari pale tu zinapohitajika bila kuwakwepa wanahabari  Katika hutuba yake hiyo makamo wa pili wa raisi amesema kwa niaba ya serikali wapotari kushirikiana na wanahabari na kuwataka wafanye tafiti mbali mbali kabla ya kuandika taarifa zao kwenye vyombo vyao wanavyofanyia kazi.  BALOZI SEIF akagusia baadhi ya nchi ambazo wananchi wake wamepoteza imani na vyombo vya haba