KUNYESHA KWA NVUA KWENYE VISIWA VYA ZANZIBAR YAWA ADHABU KWA WAKAAZI WA KINUNI

Na mwandishi wetu

Kufuatia nvua zinazoendelea kunyesha kote nchini na kusababisha maeneo kadhaa kujaa maji ikiwa ni pamoja na miundo mbinu ya bara bara kuharibika vibaya na kusababisha usafiri kuwa mgumu wa DALADALA na kupelekea wakaazi wa kinuni kulazimika kulipia nauli ya shilingi mia tano (500) tofauti na nauli ya kawaida ya shilingi mianne (400)
   Wakiongea na mwandishi wa habari hizi kwa huzuni kwenye daladala hizo abiria ambao ni wakaazi wa eneo la kinuni wamekuwa wakihoji juu ya mamlaka zinazohusika na miundombinu kuwasahau jambo linalowapa wasiwasi kuwa wamesahaulika katika taifa lao
   Kwa upande wao makondakta na madereva wa daladala hizo wamedai kuwa tayari wameshapeleka malalamiko yao juu ya ubovu wa bara bara hiyo ambo inaongoza njia za ndani kwa idadi kubwa ya abiria.
  Wamesema wao wanalipia stahiki zote za njia lakini kinacha washangaza bara bara hiyo ikiharibika wakati wa nvua hulazimika kujaza kifusi ili kupata sehemu ya kupitisha gari zao, baada ya kumaliza kujaza kifusi hupandisha bei hiyo ili kuchasha kwa njia hiyo jamii inayo ishi kwenye eneo hilo ambayo ndio watumiaji wa barabara hiyo
    Barabara ya KINUNI na MAGOGONI NDANI katika hali ya kawaida ukiambiwa inaruti mbili za gari huwezi kuamini kabisa uzima wa njia hii ni kipindi cha jua pekee na ikianza nvua gari nyingi huharibika kwa upakizi mbaya wa abiria kupita kiasi na kufanya gari chache zibakie kutoa huduma kwenye eneo hilo.
    Kwa vile eneo hilo halina trafic kuanzia kwa MABATA hadi kufika KINUNI hupakiwa abiria mithili ya mbirimbi hupati hata pakutia mguu ndani na kwenye kibao cha nyuma hukaa abiria zaidi ya nane (8) mpaka kumi na mbili (12) wakiwa wananing'inia.
   Wakaazi wa kinuni wamedai hawajapata kabisa faida ya kuwa na ruti ya gari licha ya usafiri wao kuwa HIACE CENTER ( mbavu za mbwa ) lakini hata hizo hukumbana na maneno machafu na kujazwa kupita kiasi.


Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU