ZANZIBAR CLIMATE CHANGE YAWAANDAA WANAHABARI KUWA MABALOZI WA MAZINGIRA ZANZIBAR
Na Ali Abdalla Ayoub (Bin Ghullam)
Zanzibar climate change wameandaa mafunzo ya
siku moja ya kuwajengea uwezo wa wanahabari ili kuibua maeneo muhimu ya utoaji
elimu na utetezi kuhusiana na uhifadhi wa mazingira na kukabiliana,kulindana
kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi Zanzibar
Akiongea wakati wa utoaji elimu kwa
wanahabari SOUD MOHAMMED JUMA kwenye ofisi za taasisi ya kukabiliana na athari
za mabadiliko ya tabia nchi Zanzibar ZACCA iliyopo mwanakwerekwe C wilaya ya magharibi B Unguja amesema maeneo
ambayo wameyaangalia zaidi ni pamoja na misitu,nishati,uvuvi,habari,miundombinu
na maji
SOUD
amesema kwa nchi za visiwa athari ni kubwa kutokana na kuchukuwa muda mrefu
kurejesha hali halisi ya maeneo yanayokumbwa na athari za tabia nchi huku
akipigi mfano uharibifu wa miundo mbinu kisiwani PEMBA na kimbunga kilicho
ikimba Zanzibar juzi mpaka leo imeshindikana kuweza kuweka sawa maeneo yaliyo
athirika.
Akizungumzia
suala la athari za mchanga ambao ulikuwa unachimbwa hapa Zanzibar miaka ya nyuma katika maeneo ya
mwanakwerekwe,mwakaje,donge,sebleni nk, ambapo munaleta athari hadi hiii leo amebainisha
hali hiyo na kuwataka wananchi ambao wanaishi maeneo ambayo yanachimbwa mchanga
kupanda miti ili ardhi ikae vizuri na kurejesha haiba ya maeneo yao
Comments
Post a Comment