MBUNGE WA CHAKE CHAKE YUSUF KAIZA (CUF) ALIA NA MAAFA JIMBONI KWAKE

 YUSUF KAIZA ALIA NA MAAFA JIMBONI KWAKE

Akiongea na mwandishi wetu mbunge huyo wa jimbo la chake chake YUSUF KAIZA MAKAME  amesema "Nimeskia na nimeona, baadhi ya maafa yanayoendelea kutokea kutokana na mvua zinanazoendelea kunyesha Zanzibar hasa kwenye jimbo langu LA Chake - Chake.
amesema amepokea simu kadhaa na pia ameona kwenye social media kuwa wadi ya Kibirinzi hasa maeneo ya Muharitani, Msingini, Mtoni na mengine ni maeneo yenye athari kwenye mvua zinazoendelea kunyesha". amesema kwa masikitiko makubwa kaiza
pia amese "Pamoja na maeneo hayo, naamini mvua zinazoendelea kunyesha, zimeleta athari kwenye maeneo mengi ya watu wangu wa Chake - Chake. Athari kubwa zaidi naamini ni za kijamii na kiuchumi".
akionesha hisia zake KAIZA ametaja janga hilo katika sehemu kuu mbili ambapo  1.Kijamii: wapo wanaokosa makaazi/malazi, aidha nyumba zimeanguka ama zinavujisha hasa ktk maeneo ya Muharitani na Msingini. Pia nimeona, nyumba za ibada (Miskiti) zimejaa maji mfano mskiti wa Istiqama uliopo mtoni, jambo ambalo linaleta shida kwa watu kufika na kuendelea na Ibada.
2. Kuichumi : Hali za maisha zimeendelea kuwa mbaya zaidi, kwa kuwa watu hawezi kutoka kwenda kufanya shughuli zao za kila siku za kutafuta rizki zao. Wafanya biashara wadogo na wa mboga mboga naamini hali imekuwa sio nzuri hata kidogo.
Hata hivyo YUSUF KAIZA amesema Kufuatia mvua zinazoendelea, anatoa pole kwa wote ambao wamefikwa na maafa yoyote yale kwa mvua hizi na anawaahidi kuwa wapo pamoja kwa kila hatua. Vile vile, anatoa wito kwa jamii yote ya Chake -Chake na nje kuwa karibu na wote wanaondelea kupatwa na maafa.
Pia, akatoa wito kwa Mamlaka husika kuangalia Upya, mfumo wa mitaro ya Maji taka Kwenye mji wa Chake-Chake. Kwani, maafa mengine yanasababishwa na mifumo mibovu ya mitaro na mabomba ya maji taka.


Yussuf Kaiza Makame (Mb), 

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU