HALI ILIVYO KWENYE JIMBO LA CHAKE CHAKE KUJAA MAJI KWA MSIKITI WA AFRIKANA
KUJAA MAJI KWA MSIKITI WA AFRIKANA NI MAKOSA YA WAJENZI.
Ameandika SAIDI MIRAJI ABDALLA katika ukurasa wake wa FACEBOOK kuwa "Kwa mimi niliezaliwa na kukulia katika mji wa Chake Chake Pemba na ninae vijua vyema viunga vya mji huo, hainishangazi kamwe kwa eneo lililojengwa msikiti huu hapo Miembeni maarufu Afrikana kujaa maji kihivi. Wajenzi wa msikiti huu walipaswa kujua historia ya mahali walipotumia mamilioni ya fedha na jografia yake ili wajue namna ya ujenzi uliopaswa kujengwa mahali hapo".
Pembezoni mwa msikiti huo kuna mto unaopokea maji kutoka sehemu za vitongoji, kupitia wawi, machomanne, michakaeni, shamiani, mtoni, msingini na kuyapeleka, bandataka hadi nkokota ngozi ambapo yana mwagika baharini, huko nyuma yanakotiririka maji hayo kutoka milimani husomba vitu vingi mvua zikiwa kubwa kidogo mto hujaa maji na kufurika, sababu njia yake ni nyembamba na una mchanga mwingi, hadi watu hutoa mchanga wa kujengea katika mto huo.
Tatizo jengine ni kwamba baada ya mto huo kwa pembeni kuna chem chem ya maji ya miembeni ambapo ipo katika bonde hilo hilo lenye msikiti uliojaa maji.
Kwa ujumla ukiacha hali hio ya kijiografia, kihistoria eneo lililojengwa msikiti huu ndipo mahali palipokua na mji wa miembeni chake chake ambao ulikuwa na nyumba nyingi maduka, sehemu za stsrehe nk mji huo ulighariki wote kwa mvua kama hizi, palijaa maji nyumba zikazama watu wakahama.
Baada ya kupotea kwa sura ya mji eneo hilo liligeuzwa mashamba ya mpunga ambayo nayo yalishindwa kuendelezwa kwa sababu ya kujaa maji. Hapo ndipo vijana wa maji huo kutoka timu ya Afrikana, wakaamua kufukia kwa fusi eneo hilo na kutengeneza uwanja wa mpira uliopewa jina la timu hio, katika harakati za mpira kila pakinyesha mvua uwanja huo haukuweza kutumika kwa zaidi ya miezi kutokana na kujaa maji sambamba na ule wa banda taka.
Hapo ndipo zikaja plani za kujengwa kwa msikiti huu mkubwa wa ibaadhi ambapo ulikusudiwa pia uwe na maktaba na shughuli nyengine za kiislamu.
Kwa mazingira ya kijografia, kihistoria na aina ya ujenzi uliojengwa msikiti huu katikati ya SHIMO la Afrikana hainishangazi kujaa maji wakati wa mvua na hilo sijambo geni kwa wakaazi wa maji wa chake chake.

Comments
Post a Comment