MASJID MTAMBANI YATOA TAMKO KUHUSU MAUWAJI YA KIHOLELA NA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA ZA MOTO NCHINI TANZANIA

MASJID MTAMBANI YATOA TAMKO KUHUSU MAUAJI YA KIHOLELA NA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA ZA MOTO.
Na Mwl Razaq Mtele Malilo jijini dar es salaam
Masjid Mtambani ni Msikiti uliopo maeneo ya Kinondoni Jiji Dar Es Salaam leo kupitia Imamu wa Msikiti huo umetoa tamko zito kuhusu hali ya usalama nchi hususani matumizi holela ya silaha za moto na mauaji ya mara Kwa mara ya raia na jeshi la polisi.
Imamu wa Mtambani akiwahutubia waumini waliokuwa wamehudhuria kuswali ibada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti huo wa Mtambani Leo Mei 19/2017 katika hotuba yake iliyohusu kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini pia katika hotuba yake ya pili aligusia masuala ya matumizi mabaya ya silaha za moto na mauji ya raia wasio na hatia na mauwaji ya jeshi la polisi.
Katika matumizi mabaya ya silaha za moto  Imamu aligusia kutishiwa bastora Kwa aliyekuwa Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe Nape Nnauye na kitendo cha Polisi kupiga risasi hewani kwenye tukio la aliyekuwa naibu waziri wa JK Mhe Adam Malima.
Katika hatua hiyo, Imamu amewataka wahusika kutofanya vitendo hivyo kwani vinaashiria uvunjifu wa amani na pia itapelekea wananchi kuzowea hali hiyo na hata kuzowea kuzisikia mara Kwa mara mililo ya risasi jambo ambalo litapelekea hali mbaya katika taifa.
Amewataka jeshi la polisi kutumia silaha zao Kwa uweledi na umakini ili waweze kulinda amani ya nchi 
Katika matukio ya mauaji, imamu amegusia na kuongea Kwa uchungu mkubwa mauwaji ya polisi yaliyotokea Kibiti na kukemea pamoja na kulaani vitendo hivyo vya kuwauwa polisi ambao wapo Kwa ajili ya kulinda raia na mali zao.
Pia Imamu aligusia na kuongea Kwa uchungu tukio la kuuwawa sheikh na Imamu Msaidizi wa moja ya Msikiti huko Mbagala ndugu Mohammed Almas mzaliwa wa Kilwa tukio la kuuwawa Kwake lilitokea hivi majuzi katika maeneo ya Kurasini Benki ya NMB katika jengo la Uhamiaji jijini Dar.
Imamu alieleza kuwa ndugu Almas ni kijana mwadilifu na sio jambazi Kama Polisi wanavyodai na kuongeza kuwa marehemu alikuwa ni mcha mungu ambaye hata dini yake inakemea ujambazi, wizi, na matendo mengine yaliyokatazwa katika kitabu kitukufu cha Quran na hadithi za Mtume Muhammad.
Alisema si sahihi kabisa masheikh kuhusishwa na tuhuma nzito kama hizo na kuuwawa.
 Pia aligusia ripoti ya familia kuwa bwana Almasi hakuwahi kuwa na rekodi yoyote ya uhalifu zaidi tu kwamba alikuwa mwanazuoni na mcha mungu mkubwa katika maisha yake yote aliyoishi hadi umauti unamkuta kwenye mikono ya polisi wa nchi yake aliyoitumikia kwa uzalendo mkubwa.



TAMKO
Imamu amevitaka vyombo husika Kama serikali yenyewe na Bunge kuunda tume maalumu ya kuchunguza vitendo hivi ni akina nani wanajihusisha na vutendo vya kigaidi vya kuua polisi na raia hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri ili kubaini waalifu hao na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria juu ya magaidi hao.
Lakini pia Imamu anaitaka serikali au Bunge kufanya uchunguzi ilikubaini wale watu wanaoteswa na kuuawa na polisi je, ni kweli wanajihusisha na uhalifu huo au la.
Pia Imamu alisema watu wengi wanaoteswa na kuuawa ni waislamu tena wenye ndevu jambo ambalo linatia mashaka kwamba waislamu tena maimamu ndio majambazi katika jiji la Dar na mkoani Pwani kitu ambacho Imamu amepinga Kwa nguvu zote.
Amesisitiza kuwa kuwahusisha masheikh na maimamu na ujambazi na kisha kuwaua ni jambo la kusikitisha na kuumiza hasa Kwa waislamu na kuitaka serikali au bunge kuunda tume ili ifanye uchunguzi kuhusu hali hizi na kuweka wazi kila kitu ili umma ufahamu nini kinaendelea na kuondoa sintofahamu miungoni mwa wananchi.
Aidha, Imamu amewataka waislamu wote kuwa na subira wakati huu ambao ufumbuzi wa masuala haya unatafutwa na kudumisha amani ya nchi huku akisisitiza zaidi umoja na mshikamano miungoni mwa waislamu.


Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU