UMWAGAJI TAKA OVYO MITAANI NI CHACHU YA KUENEZA MARADHI YA MIRIPUKO
Na mwandishi wetu
Katika
kuweka hali bora ya afya wananchi wanatakiwa
kuwa wepesi katika kumwaga taka kwenye makontena
ili kuepusha uzagaaji wa taka ovyo hali inayosababisha kutokea kwa maradhi mbali
mbali ikiwemo ya miripuko.
Pia akina mama majumbani na wafanya biashara wanatakiwa kuwatuma watu wenye ufahamu pindi
wanapokwenda kumwaga taka kwa usalama wa afya zao na wataifa kwa ujumla.
Wito
huo umetolewa na Afisa Mahusiano wa Baraza la Manispaa Zanzibar Haitham
Mzee Yussuf wakati akizungumza na mwandishi
wetu huku ofisini kwake malindi mjini unguja amewataka wananchi kuwa wepesi
wa kumwaga taka ili kuepusha mrundikano wa takataka na kutupwa taka hizo na
watu wenye uwelewa wa utupaji wa taka ili kuepusha kumwaga nje ya makontena au
pahala ambapo haparuhusiwi kisheria hususan kipindi hiki cha mvua zinazoendelea
kunyesha kote nchini
Hata hivyo akaitaka jamii kuwa waangalifu wa
utunzaji na utumiaji wa maji na vyakula kwani kuna taarifa za kuanza kupatikana
wagonjwa wa kipindupindu
Comments
Post a Comment