WASARIFU VYUMA WAKUTANA FAINALI
Chuo cha ufundi JKU na Chuo cha ufundi Mkokotoni watakutana fainali ya mpira wa miguu baada ya ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati na kuwaondoa mwanakwerekwe VTC kwa JKU na makunduchi kwa Mkokotoni. JKU waliwafungashia virago wachonga mbao wa kwerekwe kwa jumla ya penati 5 kwa 4 huku Mkokotoni iliwaduwaza ndugu zao makunduchi kwa bakora 4-3 katika viunga vya Dole Olympic Mkokotoni watakutana na JKU kwenye fainali kila timu ikijinasibu kutaka heshima ya kisiwa unguja