"WANAHABARI WAFUATENI MAWAZIRI WAKUPENI TAARIFA " MAKAMU WA PILI WA RAISI BALOZI SEIF ALI IDDI

WANAHABARI KUWENI HURU KUIYELIMISHA JAMII NJOONI OFISINI KWANGU
Makamo wa pili wa raisi wa serikali ya mapinduzi ya ZANZIBAR mh BALOZI SEIF ALI IDDI amewataka wanahabari kuwa huru kuandika habari zenye kujenga jamii imara bila kujali vikwazo ambavyo vinawakuta na kitaja kama changamoto za kuwajenga katika taaluma yao
   Katika maadhimisho hayo ya siku ya wanahabari duniani yaliyofanyika leo 03/05/2017 kwenye holi la chuo cha uwandishi wa habari kilimani mjini unguja BALOZI SEIF amesema raisi wa Zanzibar ambae pia ni mwenyekiti wa BARAZA la MAPINDUZI DR ALI MOHAMMED SHEIN amewataka mawaziri wote kutoa taarifa kwa wanahabari pale tu zinapohitajika bila kuwakwepa wanahabari
 Katika hutuba yake hiyo makamo wa pili wa raisi amesema kwa niaba ya serikali wapotari kushirikiana na wanahabari na kuwataka wafanye tafiti mbali mbali kabla ya kuandika taarifa zao kwenye vyombo vyao wanavyofanyia kazi.
 BALOZI SEIF akagusia baadhi ya nchi ambazo wananchi wake wamepoteza imani na vyombo vya habari ameitaja INDIA na MAREKANI kwa kutumia mifano hiyo amewataka wanahabri wa zanzibar kujiepusha na taarifa zisizo sahii ili kulinda heshma yao na taaluma ya habari
  Hata hivyo amepigia mfano wa habari zisizo kuwa na uhakika zilivyo igharimu taasisi ya kiserekali ya TBC kwa kuchukua taarifa za uwongo kwenye mtandao wa ( fake story ) habari za kubuni jambo lililopelekea baadhi ya watumishi kusimamishwa kazi kwenye chombo hicho.
   Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mjini magharibi mh AYOUB MOHAMMED MAHMOUD amesema anajivunia ailimia 95% ya vyombo vya habari vipo eneo lake la kazi hivyo akasisitiza kuendelea kutoa ushirikiano kama anawoendelea kuuwonesha kwenye tathnia hiyo ya habari na wanahabari kiujumla.
   Akijibu husu wale wanaosema yeye anapenda media amesema anafanya hivyo kutimiza wajibu wake kama walivyo agizwa na mh RAISI wa Zanzibar na kuwataka wanahabari wasichague habari ya kutoa kwenye vyombo vyao ili kutimiza ile adhma ya usawa wa kuikika na kuhabarika.

picha ya pamoja kati ya waandaaji wa maadhimisho na viongozi wa serikali 


mkuu wa mkoa wa mjini magharibi akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari


Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU