Posts

BODI YA UWEZESHAJI WIZARA YA KAZI YATAKIWA KUWA WAAMINIFU.

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto DR.   Moudline Cyrus   Castico ameitaka Bodi   ya Mfuko   wa Uwezeshaji Wananchi Ki uchumi   kufanyakazi zake kwa ushirikiano ,uaminifu na kujituma ili Mfuko huo uwe endelevu . Hayo ameyaeleza wakati akizindua Bodi hiyo huko kwenye ukumbi wa Wizara   yake Mwanakwerekwe wilaya ya Magharib   B’ Unguja. Amesema kwa kufanya hivyo Mfuko huo utafikia   malengo yake   na kutoa huduma za Mikopo kwa Wajasiriamali na Wananchi kwa ujumla. Dr. Moudline amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha Mfuko huo ilii Wananchi wake wakopeshwe   ili kutunisha fedha za miradi yao wanayoiendesha   ili kuweza kujiajiri na kujipunguzia umaskini. “Mahitaji yamekua makubwa maombi ya Mikopo yanapokelewa kila siku ,hivyo mshirikiane na Uongozi   wa Wizara ili kupata mbinu za pamoja za kutunisha fedha kupitia Mfuko huo “Ameisisitiza bodi hiyo . Halkadhalika ameitaka Bodi kujenga tabia ya k...

SEREKALI YA S.M.Z YAWANEEMESHA WANANCHI WAKE KWA MIKOPO.

JUMLA YA MIKOPO MIA NANENA KUMI NA MOJAYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MIA SABA NA THAMANINI   IMETOLEWA KWA AJILI YA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI KWA MWAKA 2019 AKIWASILISHA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 KAIMU WAZIRI WA WIZARA HIYO MH RIZIKI PEMBE JUMA AMESEMA MIKOPO HIYO IMETOLEWA KWA WILAYA ZOTE ZA UNGUJA NA PEMBA AMBAPO MIKOPO YA VIKUNDI NI 223, NA MIKOPO YA MTU MMOJA MMOJA NI 588. AMESEMA   KATI YA MIKOPO HIYO 461 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI TANO NUKTA MOJA IMETOLEWA KUENDESHA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIUCHUMI AMESEMA HATUA HIYO IMESAIDIA KUWANYANYUA KIUCHUMI WAJASIRI AMALI KATIKA MAKUNDI MBALI MBALI WAKIWEMO WANAWAKE, WATU WENYE ULEMAVU NA VIJANA. WAKICHANGIA BAJETI HIYO WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI WAMEIOMBA SERIKALI KUONGEZA KIWANGO CHA FEDHA KWA AJILI YA MIKOPO HIYO ILI IWEZE KULETA FAIDA ZAIDI KWA WANANCHI. AIDHA WAJUMBE HAO WAMEIOMBA SERIKALI KUF...

SERIKALI YA ZANZIBAR YAJIANDAA NA UJENZI WA SPITALI KUBWA YENYE CHUO NDANI YAKE.

Image
STATE HOUSE ZANZIBAR OFFICE OF THE PRESS SECRETARY PRESS RELEASE Zanzibar Mei 18, 2020 RAIS wa Zanzibar naMwenyekitiwaBaraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanza ujenzi wa hospitali ya rufaa na kufundishia huko Binguni, Wilayaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja hivi karibuni. Dk. Shein amesema hayo leowakati alipofanya ziara ya kulitembelea eneo linalokusudiwa kujenga hospitali hiyo Binguni na kupata maelezo kutoka kwa wataalamu na uongozi wa Wizara ya Afya. Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alisema kuwa Serikali iko tayari kuanza kwa ujenzi huo baada kukamilika mipango yake ya mudamrefu,   hivyo tayari imeamua ujenzi huo kuanza hivi karibuni. Rais Dk. Shein alisema ujenzi huo utafanywa na Kampuni ya Ujenzi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   kupitia fedha za mkopo ambapo kwakuanzia matayarisho yake yatafanywa kwa fedha za Serikali. Alielezakwuamaandaliziyakotayarinandiomaanaviongoziwotewa...
Image
POLICE (WAZEE WA TUNISIA) NI TIMU PEKEE ILIYOSHINDWA KUTIKISA NYAVU ZA WENGINE Timu ya police Zanzibar mpaka sasa imeshacheza michezo mitano kwenye ligi kuu soka Zanzibar ikitoka sare nne za bila kufungana ambapo mchezo wa jana wakicheza na mlandege wakikubali kipigo kibaya Cha goli tano kwa sifuri. Timu yapolisi inayofumdishwa na alikuwa kocha wa kikosi cha Zanzibar under -20 Nasour Salum kidodi wadau wakisema bado kocha huyo anaandamwa na mzimu wa Karume boys wa matokeo mabaya waliyoyapata kwenye michuano ya challenge nchini Uganda Michezo mengine aliyocheza Polisi Zanzibar (Wazee wa Tunisia) Michezo Mitano #ZanzibarPL Ni; ⚽POLISI 0️⃣-0️⃣MALINDI ⚽POLISI 0️⃣-1️⃣JKU  ⚽POLISI 0️⃣-0️⃣MAFUNZO ⚽POLISI 0️⃣-0️⃣MACHOMANE ⚽POLISI 0️⃣-5️⃣MLANDEGE  Ukiachia matokeo ya Jana ilikuwa pia ni timu ya Polisi ni  ngumu kufungika . Ligi kuu Zanzibar ambayo kwasasa inaanza kupitia kipindi kigumu kutokana na kukosa mdhamini hali inayopelekea timu za Pemba mbili kushindwa kufika unguja kwenye...

LIVERPOOL NA HATIHATI YA KUONDOLEWA KWENYE KOMBE LA LIGI:s

Liverpool ipo kwenye hatihati ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) ikiwa itabainika walimchezesha mchezaji ambaye hakuwa na sifa za kucheza kwenye mechi ya juzi Jumatano dhidi ya MK Dons kwenye ushindi wa 2-0 kwenye michuano hiyo. Liverpool inachunguzwa na wasimamizi wa michuano hiyo (EFL) kufuatia madai kuwa ilimchezesha mchezaji ambaye hakuwa amekidhi vigezo vya kushiriki kwenye michuano hiyo. Kwa maana hiyo wako hatarini kufutwa kwenye kombe hilo kabla hata ya pambano lao dhidi ya Arsenal mwezi ujao kwenye kombe hilo ikiwa mchezaji huyo ambaye mpaka sasa jina lake halijatajwa itabainika hakukidhi vigezo. Msemaji wa Liverpool amesema: "Klabu inafahamu suala la kiutawala kuhusiana na mmoja wa wachezaji wetu". "Tunashirikiana na mamlaka husika ili kutafuta ukweli wa jambo hilo na hatutatoa majibu yoyote mpaka mchakato huu ukamilike". Msemaji wa EFL, amesema; "Kwa sasa tunalishughurikia hili suala". Kama watakutwa na hatia basi EFL w...

Maahindano ya Vijana mpira wa kikapu yafika tamati.

Image
Mashindano ya mpira wa kikapu (basketball) Zanzibar kesho jumapili tanatarajiwa kumaliza kwa msimu huu wa 2019. Mashindano hayo yaliyo shirikiaha timu 5 za mkoa wa mjini magharibi zukitokea wilaya zote tatu za mkoa huo. Akiongea na VisiWani Zanzibar katibu wa kamati ya vijana ya mpira wa kikapu Zanzibar,( BAZA ) ndugu Mohammed amesema mashindano hayo yamekuwa na msisimko mkubwa kwa timu shiriki mpaka wadau wa mchezo huo. Amesema wamefungua ukurasa kwa maendeleo ya kikapu Zanzibar jambo ambalo awali vijana walikuwa wakicheza kwenye timu kubwa tofauti na umri wao. Kilele chake ni tarehe 30 mwezi wa tisa 2019 kwenye uwanja wa Mao ze Dong . Kwa mujibu wa wadau wa mchezo huo wamesema nibora kiushindani mashindano hayo kuliko ligi zote zinazo chezwa za mpira wa kikapu.
Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids? Fibroids ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha unaoota na kukua kwenye uterus. Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa. Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji. Chanzo Cha Fibroids Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kuku...