LIVERPOOL NA HATIHATI YA KUONDOLEWA KWENYE KOMBE LA LIGI:s



Liverpool ipo kwenye hatihati ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi (Carabao Cup) ikiwa itabainika walimchezesha mchezaji ambaye hakuwa na sifa za kucheza kwenye mechi ya juzi Jumatano dhidi ya MK Dons kwenye ushindi wa 2-0 kwenye michuano hiyo.

Liverpool inachunguzwa na wasimamizi wa michuano hiyo (EFL) kufuatia madai kuwa ilimchezesha mchezaji ambaye hakuwa amekidhi vigezo vya kushiriki kwenye michuano hiyo.

Kwa maana hiyo wako hatarini kufutwa kwenye kombe hilo kabla hata ya pambano lao dhidi ya Arsenal mwezi ujao kwenye kombe hilo ikiwa mchezaji huyo ambaye mpaka sasa jina lake halijatajwa itabainika hakukidhi vigezo.

Msemaji wa Liverpool amesema: "Klabu inafahamu suala la kiutawala kuhusiana na mmoja wa wachezaji wetu".

"Tunashirikiana na mamlaka husika ili kutafuta ukweli wa jambo hilo na hatutatoa majibu yoyote mpaka mchakato huu ukamilike".

Msemaji wa EFL, amesema; "Kwa sasa tunalishughurikia hili suala".

Kama watakutwa na hatia basi EFL watakabiriwa na wito wa ama kuwatoa Liverpool au kuwatoza faini.

Waandaaji wa michuano hiyo wamepewa nguvu zote za kuamua jambo linalohusiana na uchunguzi wa ukiukwaji wa sheria huku wakiwa na uwezo wa kutoa karipio, kutoza faini au kutoa adhabu nyingine kwa namna wanayoona inafaa.

Mwaka 2014, Sunderland waliepuka kuondolewa kwenye mashindano hayo, badala yake walitozwa faini kwa kumchezesha Ji Dong-Won bila ya kuwa na kibali chote cha kimataifa baada ya kuchukuliwa kwa mkopo akitokea Ujerumani.

Liverpool walichezesha kikosi kilichokuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mechi dhidi ya MK Dons huku kukiwa na mabadiliko ya wachezaji 11 kwenye kikosi hicho na ikihusisha kwa wachezaji wengi chipukizi kucheza.

Caimhim Keheller, Rhian Brewster na Harvey Elliott walipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza huku Sepp van de Berg, Herbie Kane wakitokea benchi kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha wakubwa.

Pambano lao la kuvutia mwezi ujao dhidi ya Arsenal lipo hatarini ikiwa ni moja ya mechi kwenye raundi ya nne ya michuano ya Carabao Cup, sasa lipo hatarini kwa kuwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo bado unaendelea.

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU