BODI YA UWEZESHAJI WIZARA YA KAZI YATAKIWA KUWA WAAMINIFU.
Waziri wa
Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto DR. Moudline Cyrus
Castico ameitaka Bodi ya
Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Ki
uchumi kufanyakazi zake kwa ushirikiano
,uaminifu na kujituma ili Mfuko huo uwe endelevu .
Hayo
ameyaeleza wakati akizindua Bodi hiyo huko kwenye ukumbi wa Wizara yake Mwanakwerekwe wilaya ya Magharib B’ Unguja.
Amesema kwa
kufanya hivyo Mfuko huo utafikia malengo
yake na kutoa huduma za Mikopo kwa
Wajasiriamali na Wananchi kwa ujumla.
Dr. Moudline
amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha Mfuko huo ilii Wananchi wake
wakopeshwe ili kutunisha fedha za miradi
yao wanayoiendesha ili kuweza kujiajiri
na kujipunguzia umaskini.
“Mahitaji
yamekua makubwa maombi ya Mikopo yanapokelewa kila siku ,hivyo mshirikiane na
Uongozi wa Wizara ili kupata mbinu za
pamoja za kutunisha fedha kupitia Mfuko huo “Ameisisitiza bodi hiyo .
Halkadhalika
ameitaka Bodi kujenga tabia ya kutembelea wateja wa Mfuko huo waliopo Mjini na
Vijijini Unguja na Pemba ili kuona maendeleo yao katika miradi
mbalimbali wanayoiendesha pamoja na
kuhamasisha wananchi kutumia huduma za Mfuko huo.
Bodi hiyo
ambayo ina wajimbe Sita Mwenyekiti wake ni Bi.Amina Ismail Kanduru na wajumbe ni Bw. Ali Aboud Mzee , Bi.Fatma
Iddi Ali, MHE. Ahmada Yahya Abdulwakil , Bw. Suleiman Haji Ali Bi.
Mwanahija Almasi Ali . na Bi. Abeida
Rashid Abdalla.
Comments
Post a Comment