SEREKALI YA S.M.Z YAWANEEMESHA WANANCHI WAKE KWA MIKOPO.
JUMLA YA MIKOPO MIA NANENA KUMI NA MOJAYENYE THAMANI
YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MIA SABA NA THAMANINI IMETOLEWA KWA AJILI YA KUWAWEZESHA WANANCHI
KIUCHUMI KWA MWAKA 2019
AKIWASILISHA BAJETI YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA
KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021 KAIMU WAZIRI
WA WIZARA HIYO MH RIZIKI PEMBE JUMA AMESEMA MIKOPO HIYO IMETOLEWA KWA WILAYA
ZOTE ZA UNGUJA NA PEMBA AMBAPO MIKOPO YA VIKUNDI NI 223, NA MIKOPO YA MTU MMOJA
MMOJA NI 588.
AMESEMA KATI YA MIKOPO HIYO 461 YENYE
THAMANI YA SHILINGI MILIONI TANO NUKTA MOJA IMETOLEWA KUENDESHA SHUGHULI
MBALIMBALI ZA KIUCHUMI
AMESEMA HATUA HIYO IMESAIDIA KUWANYANYUA KIUCHUMI
WAJASIRI AMALI KATIKA MAKUNDI MBALI MBALI WAKIWEMO WANAWAKE, WATU WENYE ULEMAVU
NA VIJANA.
WAKICHANGIA BAJETI HIYO WAJUMBE WA BARAZA LA
WAWAKILISHI WAMEIOMBA SERIKALI KUONGEZA KIWANGO CHA FEDHA KWA AJILI YA MIKOPO
HIYO ILI IWEZE KULETA FAIDA ZAIDI KWA WANANCHI.
AIDHA WAJUMBE HAO WAMEIOMBA SERIKALI KUFUATILIA
MADAI YA WAFANYAKAZI WA SEKTA BINAFSI
WANAOSIMAMISHWA KAZI KWA MADAI YA UWEPO WA MARADHI YA CORONA NA KUSEMA KWA
KUWA HATUA HIYO INAONGEZA UGUMU WA MAISHA KWA
WAFANYAKAZI WA SEKTA BINAFSI.
WAKATI HUO HUO WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI
WAMEPITISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA HABARI UTALII NA MAMBO YA KALE.
Comments
Post a Comment