Posts

Showing posts from August, 2026

WASARIFU VYUMA WAKUTANA FAINALI

Image
Chuo cha ufundi JKU na Chuo cha ufundi Mkokotoni watakutana fainali ya mpira wa miguu baada ya ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penati na kuwaondoa mwanakwerekwe VTC kwa JKU na makunduchi kwa Mkokotoni. JKU waliwafungashia virago wachonga mbao wa kwerekwe kwa jumla ya penati 5 kwa 4 huku Mkokotoni iliwaduwaza ndugu zao makunduchi kwa bakora 4-3 katika viunga vya Dole Olympic  Mkokotoni watakutana na JKU kwenye fainali kila timu ikijinasibu kutaka heshima ya kisiwa unguja

TULITAKA 6 TUMEPA MANNE

Image
Wachonga vitanda Wa Kwerekwe waendeleza wimbi la ushindi mashindano ya elimu bila malipo VTA. Chuo cha mwanakwerekwe VT kimepata mapumziko mazuri baada ya ushindi mnono Wa goli nne kwa mbili dhidi ya Experience Mchezo uliochezwa viwanja vya Olympic Dole majira ya saa nne na nusu asubuhi ya Leo. Mchezo huo ulioanza kwa mashambulizi kwa timu ya Chuo cha Kwerekwe nakupelekea kupata goli la mapema dakika ya kwanzaa ya mchezo huo     Mchezo uliwalazimu kuanza  kwa mchezaji Wa Chuo cha  Experience dakika 10 baadae kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kuunawa mpira mithili ya mchuzi wa chukuchiku na kuifanya icheze pungufu kwa Muda mwingi Wa Mchezo huo.   Michezo mengine iliyochezwa Leo mafundi magari wa mkokotoni wakiwafundisha kupangua gear box mafundi umeme Wa karume,kwa ushindi wa goli moja bila majibu. wafunga Bomba Wa Mombasa Al mubarak wakiteleza na ushindi wasiwoutolea jasho baada ya wajukuu Wa mama Samia Assalam kushindwa kufika uwanjani kwa wakati  H...

Mashindano ya Polisi Jamii magharibi B

MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP WILAYA MAGHARIBI B YALIENDELEA TENA LEO KWA VIWANJA VIWILI TOFAUTI.KIWANJA CHA KIEMBE SAMAKI KISAUNI FC WALIWEKA MPIRA KWAPANI HAWAKUFIKA UWANJANI NA USHINDI WA MAGOLI MAWILI NA POINT TATU WAMECHUKUA CHUKWANI BUYU FC.  KATIKA KIWANJA CHA NGOME ILIKUWA NI MPAMBANO KATI YA NEW GENERATION FC NA MILIMANI FC MATOKEO ,NEW GENERATION FC WAMESHINDA MABAO 3 NA MILIMANI WAMEPATA BAO MOJA GOLI LA MILIMANI LILIPATIKANA KIPINDI CHA PILI DAKIKA YA 70 LILIFUNGWA NA OMAR SAID NA MAGOLI YA NEW GENERATION FC YALIFUNGWA KIPINDI CHA PILI DAKIKA YA 75  LILIFUNGWA NA ABDI HASSAN NA PILI DAKIKA YA 81 LILIFUNGWA NA NASSORO ALI   NA LA TATU LILIFUNGWA NA AHMED MAHMUD DAKIKA YA 84           AIDHA MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MASHINDANO HAYO AMBAE NI MKUU WA KITUO CHA POLISI MAZIZINI SP- SALUM NGAYANA ALITUMIA MUDA MFUPI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUIMARISHA USHIRIKIANO AND ULINZI SHIRIKISHI KATIKA SHEHIA ZAO. KESHO MASHINDANO...

MAITI YANG'ANG'ANIIA JENENZA

Image
 Mvua yawapatia suluhu Al-Asaah licha ya ugeni wao mbele ya wenyeji Wa mashindano hayo Experience VTC . Mchezo Wa kwanza Wa mashindano ya elimu bila malipo kwa mkoa wa mafunzo ya Amali umekamilika kwa kugawanya alama vyuo hivyo hapo katika viunga vya MAO the Dong asubuhi ya Leo. Katika Mchezo huo ulishuhudia mchezaji  chuo cha.Experience akiwa Wa kwanzaa kupigwa umeme akiyaanza vibaya mashindano hayo kwa ajili ya kunusuru timu yake kupata aibu mbele ya vyuo mbali mbali vilivyokuepo uwanjani hapo. Mechi Nyengine zitachezwa hapo kesho kwa michezo miwili Mubarrak Al Mazrui vs Makunduchi ,JKU vs Adult Forodhani Karume vs ICPS , Al-Asaah VTC vs Kwerekwe