Wizara ya afya Zanzibar kwa kushirikian na taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION
wameendesha kambi ya matibabu ya midomo wazi katika hospitali ya mkoa Lumumba ikiwa ni
muendelezo wa kambi zinazofanywa na taasisi hio ili kuhakikisha watoto wenye tatizo la midomo
wazi wanapatiwa matibabu.


Akizungumza katika kambi hio Mkurugenzi na muazilishi wa Taasisi hio Dr Piter Mabula amesema
takriban miaka kumi na moja taasisi hio imekua ikitoa huduma hio na imefanikiwa kufanya
matibabu wa watu zaid ya 2500 kwa Tanzania bara na visiwani ambapo kwa zanzibbar zaid ya watu
200 wamepatiwa huduma hio Dr Piter Mabula Mkurugenzi wa taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION
Kwa upande wake Dr Sumaiya Said Abud kutoka katika hospitali ya mkoa Lumumba amesema kambi
hio ya siku tano inatarajia kufanya matibabu ya watoto 25 ambao tayar watoto hao wamefanyiwa
uchunguzi wa awali Dr Sumaiya Said Abud hospitali ya mkoa Lumumba
Sambamba na hayo sumaiya ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye tatizo la
mdomo wazi kuwafiikisha katika hospitali hio ili kupatiwa matibabu Dr Sumaiya Said Abud hospitali ya mkoa Lumumba
Nao wazazi wa watoto waliopatiwa huduma hio wameishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar
pamoja na taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION kwa kuwapatia huduma hio bure hali ambayo
inawapa faraja ya watoto wao, 


leyla Saidi Mkoa mama wa mtoto
MUONGOZO
KAMBI YA MATIBABU YA MDOMO WAZI KATIKA HOSPITALI YA MKOA LUMUMBA



Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU