TULITAKA 6 TUMEPA MANNE



Wachonga vitanda Wa Kwerekwe waendeleza wimbi la ushindi mashindano ya elimu bila malipo VTA.
Chuo cha mwanakwerekwe VT kimepata mapumziko mazuri baada ya ushindi mnono Wa goli nne kwa mbili dhidi ya Experience Mchezo uliochezwa viwanja vya Olympic Dole majira ya saa nne na nusu asubuhi ya Leo.
Mchezo huo ulioanza kwa mashambulizi kwa timu ya Chuo cha Kwerekwe nakupelekea kupata goli la mapema dakika ya kwanzaa ya mchezo huo  


 Mchezo uliwalazimu kuanza  kwa mchezaji Wa Chuo cha  Experience dakika 10 baadae kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kuunawa mpira mithili ya mchuzi wa chukuchiku na kuifanya icheze pungufu kwa Muda mwingi Wa Mchezo huo. 


Michezo mengine iliyochezwa Leo mafundi magari wa mkokotoni wakiwafundisha kupangua gear box mafundi umeme Wa karume,kwa ushindi wa goli moja bila majibu. wafunga Bomba Wa Mombasa Al mubarak wakiteleza na ushindi wasiwoutolea jasho baada ya wajukuu Wa mama Samia Assalam kushindwa kufika uwanjani kwa wakati 
Hivyo kupeleke wafunga mifereji Wa Mombasa kupewa ushindi Wa goli mbili bila.
Michezo hiyo itasimama kupisha sikukuu ya maulidi ya mazazi Mtume Muhammad SAW na kupendelea tena alhamis ya tarehe 27/8/2026 mechi moja ikipigwa katika kiwanja cha dole kati ya mkokotoni na ICPS na moja kati ya wajukuu Wa Mama Samia dhidi ya Wachonga Vihenge Makunduchi katika dimba jipya la Unguja Ukuu 


Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU