Posts

Showing posts from June, 2020

You tube imejaribu mfumo wa video ndogo kwenye simu za Smart.

YouTube Testing TikTok-Like Short Video Format on Android, iOS..! 📲 YouTube is testing a new feature on its mobile apps that will allow users to create and upload short 15-second clips, similar to TikTok. The feature is currently available to limited users, and a mass rollout can be expected after the testing phase is over. The development was announced by YouTube on its support website. In April, a report had indicated the arrival of this feature, adding that the company may call it 'YouTube Shorts.' 📲 The Alphabet-owned video platform in a post explains that the feature will allow creators to record multiple clips directly in the YouTube mobile app and upload as one video. If the video is less than 15 seconds long, it can be directly uploaded on to the platform, after recording. However, if the user wishes to upload a clip longer than 15 seconds, it needs to be uploaded from the phone gallery, the company adds.  📲 As mentioned, this feature is currently limited to se

KUELEKEA KUENDELEA KWA LIGI KUU ZANZIBAR KESHO JIONI NI SEMINA ELEKEZI

Image
NA:  ALI GHULLAM Shirikisho la mpira wa miguu visiwani Zanzibar (ZFF) likishirikiana na Madaktari wanaoshughulikia na janga la COVID-19  watafanya semina elekezi juu ya nmna ya kuingia na kusimamia michezo wakati ligi kuu ikirejea kwa wale watakao ruhusiwa kuingia viwanjani. Ameyasema hayo kaimu katibu mkuu wa shirikisho la mpira Zanzibar ndugu ALI AMEIR VUAI wakati akizungumza na VISIWANI ZANZIBAR BLOG ofisini kwake AMANI mjini Zanzibar amesema semina hiyo itafanyika saa kumi jioni kwenye uwanja wa AMANI na kushirikisha viongozi wa vilabu, Waandishi wa habari za michezo, Waamuzi, wasimamizi wa viwanjani, Wafanyakazi wa shirikisho la mpira na makocha ili kucheza mpira katika mazingira salama. Amesema semina hiyo ni miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa siku ya jumanne kwenye kikao cha madaktari wa vilabu waliokaa kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo walipokwenda kupewa miongozo ya namna ya utekelezaji wa majukumu yao viwanjani ikiwa Dunia inaendelea kusimama kwa janga

Unatumia Simu za Kiganjani Je unazifahamu Soma Hii ujue.

Image
Zifahamu kampuni bora za simu Duniani kwa 2020 Ww unatmia ipi? Mimi natumia OPPO 1: SAMSUNG . Ni kampuni ya vifaa umeme iliyopo Korea Kusini. Wana shika nafasi ya 1 kutokana na ubora wa simu zao kama; Galaxy S20, Galaxy S11, Note 10 n.k. 2: HUAWEI . Hii ni kampuni kutoka China waanzilishi wa teknolojia ya 5G. Wana matoleo MaTaTa ya simu kama; Huawei P30 Pro, Mate X, Mate 20 Pro n.k. Pato lao ni $ 121.71 kwa mwaka 3: APPLE iPHONE . Hii ni kampuni kutoka Marekani ambayo ina mfumo wake wa kipekee wa kuendesha simu zao iOS. Wana simu kama; iPhone 11 Pro, iPhone X, iPhone XR n.k. Pato lao ni $33.3 kwa robo ya mwaka. 4: XIAOMI (MI) . Hii ni kampuni nyingine kutoka China. MI inasimama badala ya Mobile Internet, wamewekeza kwenye simu, Tv, Viatu n.k. Wana simu kama; Xiaomi Mi9, Xiaomi 8 Pro, Mi Mix 3 n.k. Pato ni $ 494 kwa theluthi ya mwaka. 5: OPPO . Hii ni kampuni nyingine kutoka China ilianzishwa mwaka 2016. Ipo pamoja na Vivo, One plus na Realme. Wana simu kama; Oppo A31, F15, A5, A9

Wizara ya Elimu Zanzibar yakubaliana na Tume ya haki za binaadamu

Image
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na viongozi wa Tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora Waziri wa Elimu Bi Riziki Pembe Juma akipokea Kitabu Katibu mkuu wizara ya Elimu Dr Idrissa Muslim Hijja akipokea Kitabu kutoka kwa wazi Dr Idrissa Muslim Hijja katibu mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma  amesema Wizara ipo tayari  kushirikiana na Tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora kutoa Elimu katika Vyuo na Skuli katika ngazi mbali mbali ili jamii itambue haki na wajibu wao. Amezungumza hayo katika kikao cha Tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora kwa viongozi wa Wizara ya Elimu huko Mazizini katika  ukumbi wa Wizara hiyo, amesema ni jambo la faraja kwa Wanafunzi kuweza kujua haki zao tokea wanapoanza kusoma Elimu ya awali. Aidha Mhe Riziki ameiomba Tume hiyo kuhakikisha wanakuwa makini na kesi za udhalilisha ili watakaoathirika wapate haki zao Kama zinavyostahiki. N

Huduma bora za upatikanaji wa wa Maji na umeme mijini na vijijini ndio Dira ya SMZ.

Image
Balozi Seif Ali Iddi akitoa neno kwenye uzinduzi Makamo wa pili wa serekali ya mapinduzi zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtwisha maji mkaazi “WAHANDISI WAZALENDO LAZIMA WAJENGE HESHIMA KATIKA KUTEKELEZA MIRADI” BALOZI SEIF Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Wahandisi wa Ujenzi Wazalendo lazima wajenge Heshima wakati wa kutekeleza Miradi wanayokabidhiwa katika misingi ya uaminifu kitendo kitachowajengea SIFA na hatimae kuaminika Zaidi. Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Tangi kubwa la kuhifadhia Maji safi na salama katika Kijiji cha Kitope Mbaleni ambao ulichelewa kukamilika katika muda uliopangwa ambapo alilazimika kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” kuchukuwa hatua zinazostahiki dhidi ya Wahandisi wa Ujenzi wa Mradi huo. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza na kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” kwa usimamizi mzuri wa Mradi huo uliokuwa ukisuasua katika utekelez

Wizara ya Elimu yatoa muongozo Vyuo Vikuu

Wizara ya Elimu yatoa muongozo Vyuo Vikuu

Image
Mkuu wa kitengo Cha Uratib wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu na Mafunzo  ya Amali Zanzibar Bi Aida Juma Maoulid amewataka Wakuu wa Vyuo nchini kuhakikisha Wanafunzi wanapata Elimu ya kutosha juu ya kujikinga na Covid 19. Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika Vyuo Vikuu mbalimbali vya Unguja   kuangalia utaratibu wa ufundishaji  katika kipindi hiki Cha maradhi ya Corona. Amesema ipo haja kwa  Vyuo kutoa Elimu kwa kutumia vipeperushi  vyenye miongozo  ya kujikinga na korona ili kuendelea kuondosha kabisa maradhi hayo nchini. Nao Wakuu wa Vyuo wamesema bado jitihada ya kuelimisha Wanafunzi inahitajika hasa katika suala la uvaaji wa barakoa wanapokuwa katika mazingira ya Chuo na hata sehemu nyengine ili kuhakikisha maradhi hayo hayawapati. Aidha wamesema katika Vyuo vyao wanaandaa kamati maalum za Wanafunzi ili kusaidia kuhamasishana juu ya kujikinga na maradhi hayo. Wamesema kutokana na wingi wa Wanafunzi wameandaa utaratibu maalum wa usomeshaji ikiwemo kutumia kumbi kubwa za v