Wizara ya Elimu Zanzibar yakubaliana na Tume ya haki za binaadamu
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na viongozi wa Tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma amesema Wizara ipo tayari kushirikiana na Tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora kutoa Elimu katika Vyuo na Skuli katika ngazi mbali mbali ili jamii itambue haki na wajibu wao.
Amezungumza hayo katika kikao cha Tume ya haki za binaadamu na Utawala Bora kwa viongozi wa Wizara ya Elimu huko Mazizini katika ukumbi wa Wizara hiyo, amesema ni jambo la faraja kwa Wanafunzi kuweza kujua haki zao tokea wanapoanza kusoma Elimu ya awali.
Aidha Mhe Riziki ameiomba Tume hiyo kuhakikisha wanakuwa makini na kesi za udhalilisha ili watakaoathirika wapate haki zao Kama zinavyostahiki.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya haki za binaadam na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema Tume imeteuliwa kwa lengo la kulinda haki za binaadam na kujua misingi ya Utawala Bora.
Jaji Mwaimu amesema wapo mbioni kuhakikisha katika kila Skuli na Vyuo mbalimbali kuona kunaazishwa klabu za haki za binaadam ili kupunguza kesi za ukiukwaji wa haki za binaadamu nchini.
Pia amesema Tume hiyo inapaswa Serikali kutambua mapungufu yanayojitokeza katika Sheria mbalimbali ili kuweza kuzipatia ufumbuzi
Katika kikao hicho Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mwaimu amemkabidhi Mhe Riziki kitabu Chao Cha mpango kazi wa kutimiza majukumu yao.
Comments
Post a Comment