KUELEKEA KUENDELEA KWA LIGI KUU ZANZIBAR KESHO JIONI NI SEMINA ELEKEZI
NA: ALI GHULLAM
Shirikisho la mpira wa miguu visiwani Zanzibar (ZFF) likishirikiana na Madaktari wanaoshughulikia na janga la COVID-19 watafanya semina elekezi juu ya nmna ya kuingia na kusimamia michezo wakati ligi kuu ikirejea kwa wale watakao ruhusiwa kuingia viwanjani.
Ameyasema hayo kaimu katibu mkuu wa shirikisho la mpira Zanzibar ndugu ALI AMEIR VUAI wakati akizungumza na VISIWANI ZANZIBAR BLOG ofisini kwake AMANI mjini Zanzibar amesema semina hiyo itafanyika saa kumi jioni kwenye uwanja wa AMANI na kushirikisha viongozi wa vilabu, Waandishi wa habari za michezo, Waamuzi, wasimamizi wa viwanjani, Wafanyakazi wa shirikisho la mpira na makocha ili kucheza mpira katika mazingira salama.
Amesema semina hiyo ni miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa siku ya jumanne kwenye kikao cha madaktari wa vilabu waliokaa kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo walipokwenda kupewa miongozo ya namna ya utekelezaji wa majukumu yao viwanjani ikiwa Dunia inaendelea kusimama kwa janga la CORONA.
VUAI amesema wataalamu hao wakimaliza semina hiyo kwa pande zote zitakuwa tayari kufika viwanjani kwa usalama na kujikinga na maambukizi sambamba na kukinga maambukizi yasienee kwa wengine.
Comments
Post a Comment