Huduma bora za upatikanaji wa wa Maji na umeme mijini na vijijini ndio Dira ya SMZ.

Balozi Seif Ali Iddi akitoa neno kwenye uzinduzi
Makamo wa pili wa serekali ya mapinduzi zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtwisha maji mkaazi

“WAHANDISI WAZALENDO LAZIMA WAJENGE HESHIMA KATIKA KUTEKELEZA MIRADI” BALOZI SEIF

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Wahandisi wa Ujenzi Wazalendo lazima wajenge Heshima wakati wa kutekeleza Miradi wanayokabidhiwa katika misingi ya uaminifu kitendo kitachowajengea SIFA na hatimae kuaminika Zaidi.

Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo alipofanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Tangi kubwa la kuhifadhia Maji safi na salama katika Kijiji cha Kitope Mbaleni ambao ulichelewa kukamilika katika muda uliopangwa ambapo alilazimika kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” kuchukuwa hatua zinazostahiki dhidi ya Wahandisi wa Ujenzi wa Mradi huo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimpongeza na kumshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” kwa usimamizi mzuri wa Mradi huo uliokuwa ukisuasua katika utekelezaji wake.

Akitoa Taarifa ya Mradi huo  Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Youth Icon inayosimamia Ujenzi huo kwa ufadhili wa Taasisi moja ya Umoja wa Mataifa Bwana Abdullah Suleiman amesema jumla ya Shilingi Milioni 10,000,000 tayari zimeshalipwa katika Awamu ya pili ya Mradi huo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Rajab Ali Rajab amesema alilazimika kumpa agizo la kuripoti kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaskazini “B” Asubuhi ya Ijumaa ya Tarehe17 Aprili Mwaka huu Mkurugenzi wa Kampuni ya Grative Tanzania Limited yenye Makao Makuu yake Dar es salaam kutoa maelezo ya kina kuhusiana na kuchelewa kumalizika kwa wakati Mradi huo.

Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezindua Rasmi Kisima cha Maji Safi na salama kilichojengwa na Uongozi wa Jimbo la Mahonda kwa Ufadhili wa Taasisi ya Misaada ya Hayrat Yardin kilichopo Magharibi ya Skuli ya Mahonda.
 
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Juni 08, 2020.
 


Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU