UMSHIRIKIANO BAINA YA KINA MAMA WENYEWE KWA WENYEWE NI NJIA YA MAENDELEO NA USHINDI MKWA
WANAWAKE WA CCM WILAYA YA KATI WAMETAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA MASHIRIKIANO NA MAELEWANO KWA LENGO LA KUKILETEA MAFANIKIO CHAMA HICHO. KAULI HIYO IMETOLEWA KATIKA TAWI LA CCM TUNGUU NA DIWANI WA KUTEULIWA NDUGU SALUM KHAMIS KIBESHI WAKATI ALIPOKUWA AKIUFUNGUA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WANAWAKE U.W.T JIMBO LA TUNGUU. AMESEMA MASHIRIKIANO NA UMOJA KWA WANAWAKE WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDIO NJIA PEKEE ITAKAYOPELEKEA KUIMARIKA KWA CHAMA HICHO NA KUKIPATIA USHINDI MKUBWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020. AIDHA AMEWATAKA WALE AMBAO HAWAKUFANIKIWA KUPATA KURA ZA KUTOSHA KATIKA UCHAGUZI HUO KUACHANA NA MAKUNDI NA BADALA YAKE KUWA KITU KIMOJA NA KUTOA MASHIRIKIANO YA KUTOSHA KWA VIONGOZI WAPYA WALIOCHAGULIWA ILI KUPELEKA MBELE MAENDELEO YA CHAMA HICHO. WAJUMBE WA MKUTANO HUO MKUU WAMEMCHAGUA NDUGU BAHATI ISSA SULEIMAN KUWA MWENYEKITI WA U.W.T JIMBO LA TUNGUU KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO. AIDHA PIA WAMEWACHAGUA WAJUMBE 4 WA MKUTANO MKUU MKOA, WAJUMBE 2 MKUTANO MK...