SEREKALI YATAFUTA MUARUBAINI WA MRUNDIKANO WA KESI MAHAKAMANI

MKOA WA KUSINI UNGUJA

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA KUSHIRIKIANA NA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA IMECHUKUA HATUA NZITO YA KUIFANYIA MAREKEBISHO SHERIA YA USHAHIDI SURA YA TISA YA MWAKA 2016  KWA LENGO LA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI KWA WANANCHI MAHAKAMANI .



KATIBU WA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA ZANZIBAR NDUGU ASMA JIDAWY AMETOA KAULI HIYO KATIKA AFISI YA MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA TUNGUU WAKATI ALIPOKUWA AKIFAFANUA BAADHI YA VIFUNGU VYA SHERIA MPYA YA USHAHIDI KWA MAHAKIMU, WAENDESHA MASHTAKA PAMOJA  NA WASAIDIZI WA SHERIA WA MKOA HUO.    

AMESEMA UTEKELEZAJI WA SHERIA HIYO ITAONDOSHA MALALAMIKO KWA WANANCHI KUTOKANA NA KWAMBA IMEZINGATIA KUKUBALIKA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA PAMOJA NA KUYAHUSISHA MAKUNDI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM WAKIWEMO WAGONJWA WA AKILI JAMBO AMBALO LITAIMARISHA UTEKELEZAJI NA UTENDAJI BORA KATIKA VYOMBO VYA MAHAKAMA SAMBAMBA NA KUIMARISHA SERA NA UTAWALA BORA.

HIVYO AMEWATAKA MAHAKIMU KUWA MAKINI NA KUTUMIA MBINU MBADALA NA RAFIKI  WAKATI WANAPOKUWA WAKIHUKUMU KESI HUSUSAN KWA MAKUNDI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM PIA NA KUWATAKA WANANCHI KUUNGA MKONO JUHUDI HIZO ZA SERIKALI ILI KUONA KWAMBA LENGO LILILOKUSUDIWA LINAFIKIWA.


NAO WASHIRIKI MKOANI HUMO WAMEIPONGEZA JUHUDI ZILIZOFIKIWA NA TUME HIYO KWA KUFANIKIWA KUIFANYIA MAREKEBISHO SHERIA MPYA AMBAYO ITAWASAIDIA WANANCHI KWA KIASI KIKUBWA KUPATA HAKI KWANI SHERIA HIO IMEZINGATIA  UTOAJI WA HUKUMU KWA NJIA ZA KIELETRONIKI


Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU