UFUGAJI WA NYUKI KIWE KICHOCHEO CHA KUONDOA MARADHI NA UMASIKINI MKOA WA KUSINI UNGUJA
NA .MAUA/FATMA MKOA WA KUSINI UNGUJA
MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA DKT
IDRISSA MUSLIM HIJJA AMESEMA SERIKALI MKOANI HUMO ITAENDELEA NA JUHUDI ZA
KUWASHAJIHISHA WANANCHI KUENDELEA KUTUMIA MBINU ZA KISASA ZA UFUGAJI WA NYUKI
AMBAO UTAWAPATIWA TIJA ZAIDI NA KUJIKWAMUA NA HALI NGUMU ZA MAISHA.
DKT IDRISSA AMETOA KAULI HIO HUKO
MAKUNDUCHI WAKATI ALIPOKUWA AKIFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA NYUKI
NA KUANGALIA KAZI ZA UFUGAJI WA NYUKI
KWA NJIA ZA KISASA MKOANI HUMO AMBAPO
VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WANAJUMUIYA WA UFUGAJI NYUKI KUTOKA VIJIJI MBALI
MBALI VILIVYOMO NDANI YA MKOA HUO WAMESHIRIKI KATIKA KONGAMANO HILO.
DKT IDRISSA AMESEMA SERIKALI
IMEAMUA IMEAMUA KUCHUKUA HATUA HIO KWA KUZINGATIA KWAMBA WAKATI UMEFIKA KWA
WANANCHI WA MKOA HUO KULIPA KIPAUMBELE SUALA LA UFUGAJI WA NYUKI KWA KUTUMIA
MBINU YA KISASA KUTOKANA NA KWAMBA WANAZO RASILIMALI ZA KUTOSHA IKIWEMO UKUBWA
WA MAENEO YENYE MITI MINGI YENYE UOTO WA ASILI JAMBO AMBALO LITAJENGA MAZINGIRA
MAZURI YENYE UZALISHAJI MKUBWA WA MAZAO BORA YA NYUKI.
HIVYO AMESISITIZA HAJA KWA
WANANCHI KUWATUNZA NA KUWAHIFADHI NYUKI SAMBAMBA NA KUZICHANGAMKIA FURSA
ZILIZOPO ILI KUIMARISHA HALI YA UKUAJI WA KIPATO KWA MWANANCHI MMOJA MMOJA NA
TAIFA KWA UJUMLA.
AIDHA AMEZIPONGEZA JUHUDI
ZINAZOCHUKULIWA NA WANANCHI, WAHISANI PAMOJA NA JUMUIYA YA WAFUGAJI NYUKI
ZANZIBAR (ZABA) KATIKA KUFANIKISHA UZALISHAJI WA ASALI BORA NA YENYE KIWANGO.
KATIKA RISALA YAO WANAJUMUIYA HAO
WAMESEMA PAMOJA NA MAFANIKIO WALIYOPATA LAKINI BADO WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO
MBALI MBALI KAMA VILE UINGIAJI WA WADUDU
AINA YA KUNGUNI KWENYE MIZINGA, UHARIBIFU WA MAZINGIRA YA MISITU, WIZI WA ASALI
NA UCHOMAJI MOTO NYUKI NA MISITU.
NAE NAIBU KATIBU WA JUMUIYA YA
WAFUGAJI NYUKI ZANZIBAR NDUGU ABDU BARUWANI AMESEMA TANGU KUANZISHWA KWA
UTUMIAJI WA MBINU ZA KISASA ZA UFUGAJI WA NYUKI WAMEWEZA KUPIGA HATUA KUBWA ZA
MAENDELEO KWANI WAMEWEZA KUZALISHA MAZAO YENYE UBORA NA THAMANI NA KUKUBALIKA
KATIKA MASOKO YA NDANI NA NJE.
Comments
Post a Comment