MIKAKATI YA UGATUZI MKOA WA KUSINI UNGUJA YAIVA
MKOA WA KUSINI UNGUJA
MAAFISA WA ELIMU NA WALIMU WAKUU WA SKULI ZA MAANDALIZI NA
MSINGI MKOA WA KUSINI UNGUJA WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA MASHIRIKIANO NA KUA
KARIBU NA WAKURUGENZI WA HALMASHARI KWA
LENGO LA KUZITATUA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZOIKABIL SEKTA
HIYO.
MKURUGENZI WA
HALMASHAURI YA WILAYA YA KATI NDUGU MOH.D SALUM AMETOA KAULI HIYO SKULI YA
KIBELE WAKATI ALIPOKUA AKIZUNGUMZA NA WALIMU WAKUU NA MAAFISA WA ELIMU MKOANI
HUMO KATIKA MAFUNZO ELELEKEZI JUU YA MPANGO WA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI
ZA MITAA KUFUATIA KUTEKELEZWA MPANGO WA
SERIKALI WA KUKASIMU MADARAKA KUTOKA SERIKALI KUU KWENDA SERIKALI ZA
MITAA.
AMESEMA MASHIRIKIANO YA KARIBU KATI YA HAMASHAURI NA SEKTA YA
ELIMU NDIO NJIA PEKEE ITAKAYOWEZESHA KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO MBALI MBALI
ZIKIWEMO UKOSEFU WA HATI MILIKI KWA BAADHI YA SKULI , UHABA WA WALIMU, PAMOJA
NA POSHO ZA SAFARI NA LIKIZO HIVYO NI VYEMA WAKAONA KWAMBA WALIMU HAO
WANAKUWA NA MIPANGO NA MIKAKATI
MADHUBUTI ITAKAYOFANIKISHA MPANGO HUO NA KUFIKIA MALENGO.
NAE AKIWASILISHA MADA JUU YA DHANA YA KUWEPO KWA SERIKALI ZA
MITAA MKURUGENZI MIPANGO, SERA NA UTAFITI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA,
SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ NDUGU DAIMA MOH’D MKALIMOTO AMESEMA
LENGO LA SERIKALI KUANZISHA MPANGO HUO NI KURAHISISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA
KIJAMII NA KULETA USAWA NA UFANISI KATIKA NYANJA MBALI MBALI ZA KUJILETEA
MAENDELEO AMBAPO AMEWATAKA WALIMU HAO KUONDOA HOFU NA KUTEKELEZA VYEMA MPANGO
HUO.
NAO WALIMU HAO WAMEELEZEA MATUMAINI YAO KWAMBA IWAPO MPANGO
HUO UTATEKELEZWA KAMA ULIVYOPANGWA KUNA UWEZEKANO MKUBWA KUIMARIKA KWA SEKTA YA
ELIMU NA KULETA MABADILIKO.
Comments
Post a Comment