NEEMA YAWASHUKIA WAFANYAKAZI WASTAAFU WA SMZ
SMZ YAONGEZA PENCHENI
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeongeza kiwango cha pencheni kwa wastaafu wa kima cha chini kuanzia mwezi huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Waziri wa Fedha na Mipango Dk Khalid Salum Mohammed amesema wastaafu hao watalipwa shilingi 90,000 kila mwezi ikiwa nyongeza ya shilingi 40,000 waliyokuwa wakilipwa.
Waziri huyo wa Fedha na Mipango alisema kwamba kuna wastaafu 12182 nao wamepata nyongeza ya shilingi 50,000 katika pencheni wanayopata kwa mwezi ambapo nyongeza hiyo itaanza mwezi huu.
Dk Khalid alisema kwamba Serikali imeamua kuongeza kiwango cha malipo ya pencheni kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha wastaafu kuwajengea mazingira bora zaidi ya maisha baada ya kustaafu.
Alisema serikali imeshajadili na kupitisha mabadiliko ya pencheni kwa wastaafu na sasa tayari mapitio yameshakamilika mwanzoni mwa mwezi huu hivyo , hatua za kuanza malipo hayo yataanza.
“Tunajitahidi kuongeza kiwango hicho kadri hali itakavyokuwa inaruhusu, dhamira ya Serikali ni kuona kila wastaafu wetu wanaendelea kufurahia maisha hata baada ya kustaafu utumishi wa umma” Alisema Waziri huyo wa Fedha na Mipango.
Alisema ingawa mabadiliko hayo yalitarajiwa kuanza mwezi wa Julai yalichelewa kutokana kutokamilika kwa marekebisho na mapitio kwa wastaafu hao hivyo kuanzia mwezi huu wastaafu wote watapokea kuanzia 90,000 kwa mwezi.
Akizungumzia kuhusu wastaafu waliokuwa na nyadhifa za uongozi katika utumishi wao , Waziri wa Fedha na Mipango alisema serikali tayari imefanya mapitio kwa wastaafu hao na kuanza kufanya marekebisho kwa utaratibu utakaweza kuwaweka katika haki inayostahiki.
“Waliokuwa na nyadhifa za uongozi pencheni zao zitarekebishwa Serikali inafanya utaratibu ili na wao waweze kupata nyongeza inayostahiki ili waweze kwenda sambamba na hali iliopo sasa ya kupata pencheni inayokubalika kwao,” alieleza Waziri Dk Khalid
Alisema Serikali inachukua juhudi kubwa za kuwanyanyua watumishi wa Umma na wastaafu wake kwa kuwaongeza mishahara na pencheni kwa lengo la kuwasidia na kuongeza juhudi katika utumishi pamoja na kuleta maendeleo nchi ili kuweza kukuza kipato nchini.
“Mafanikio haya na juhudi zinazochukuliwa na serikali ziungwe mkono ili ziweze kuleta tija katika kukuza uchumi, pato la serikali liongezeke na haya yote yanafanywa ili kuinua kipato cha nchi’” alieleza Waziri wa Fedha.
Itakumbukwa kuwa Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa Serikali kutoka shilingi 150,000 hadi kufikia shilingi 300,000 kwa mwezi.

Comments
Post a Comment