Posts

Historia ya Majestic cinema.

Image
Historia Ya Majestic Cinema Na  Kuunguwa  Moto. Majestic Cinema, iliyofunguliwa mnamo Oktoba 20, 1955, baada ya jengo la kwanza la sinema kuunguwa, ilikuwa ni fahari ya Zanzibar, Ilibuniwa na mbunifu maarufu  Mzanzibari Dayalji Pitamber Sachania, baada ya sinema ya awali, Royal Cinema iliyojengwa 1921, kuteketea kwa moto mnamo Februari 8, 1954 ,siku hiyo kulikuwa na Zanana show ,ingawa nje kulikuwa na mabarobaro tele wakitia macho nuru, siku ambayo ikiendeshwa filamu inayoitwa Albela.Albela ni filamu ya vichekesho na  muziki ya Bollywood ya 1951 iliyoongozwa na nyota Bhagwan Dada na Geeta Bali. Sinema  Yakihindi ilikuwa ya  kwanza kwa  mapato ya juu kwa wakati huo na sinema ilijaa wanawake ikaleta mtafaruku mkubwa  . Royal Cinema, iliyokuwa sinema ya kwanza ya kifahari katika Afrika Mashariki, ilifunguliwa na Hassanali Adamjee Jariwalla na kubuniwa na J.H. Sinclair,  Majestic Cinema ilikuwa na muundo  mpya wa kipekee wa vishubaka vya mis...

Photo from Ali Ghullam

Image
Petroleum imepanda kwa shilling mia moja na mbili kwa bei mpya ya mwezi wa tisa, ambapo bei ya awali ilikua ni 3063 , wakati bei ya diesel imeshuka kwa shilling kumi na mbili ambapo awali ilikua ikiuzwa kwa shilling 3259 na bei ya mafuta ya taa ikibaki kawa ilivyo haikuongezeka wala kupanda. Bei ya mafuta ya ndege yakushuka kwa shillings sita ambapo yalikuwa yakiuzwa kwa shs 2843. Hii imetokana na taarifa zinazo tolewa na mamlaka ya maji na nishati Zanzibar ZURA leo tarehe 8 September 2024 huko ofisini kwao maisara mjini Unguja.

KUELEKEA MCHEZO WA MUEMBE MAKUMBI NA NEW CITY TAMBO HIZI APA.

Image

Jeshi la polisi Tanzania latoa tahadhari hii.

Image

Michezo inawajenga kiakili wanafunzi na wazee wao.

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, amewataka walimu na wazazi kushirikiana katika kukuza na kulea vipaji vya wanafunzi. Hayo ameyaeleza wakati akifunga   Tamasha la tatu la Michezo la Skuli ya Leera la mwaka 2024 lililofanyika  kwenye uwanja wa Amani Complex . Alisema watoto hao watakapoekewa mashirikiano baina pande zone mbili watakuja peperusha bendera ya Taifa katika kuimarisha michezo. Aliwataka skuli ya Leera kuendelea kuibua vipaji kwani miundo mbinu ya michezo inaendelea kukua kwa kasi zaidi pia ni vyema kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa jitihada za kuimarisha sekta ya Michezo nchini. Waziri Tabia alieleza Serikali imetenga fedha billion 70 katika sekta ya michezo, hivyo hawanabudi kuthamini michezo na kuiendeleza katika skuli kwa watoto wao. Akisoma risala ya Skuli hiyo  Mkuu  wa  Utawala Jonathan Kahatano, alisema skuli hiyo inatoa taaluma bora ikiambatana ...

ALMUBARAK na ZOI wakubali kuwa madaraja ya fainali.

Image
Baada ya kukubali kipigo cha goli moja bila chuo cha Almubarak almazruwi kutoka kwa Mafundi umeme wa magomeni makada chuo cha Microtech kesho wata ,  jitupa uwanjani kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya watembeza watalii wa Amani ZOI language waliofanywa daraja na chuo cha Microtech kwa kutandikwa bakora mbili bila majibu. Kesho asubuhi ZOI na Almubarak watacheza kujua nafasi ya tatu na ya nne. Mchezo wa fainali utapigwa Mao ze Dong siku ya Jumapili hii ikiwakutanisha ICPS wakiumana na Microtech.

WALIWOONGOZA KWENYE MAKUNDI WAKWAMA KWA NAMBA NNE.

Image
Mashindano ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo na vituo vya mafunzo ya amali yameingia hatua ya nusu fainali baada ya kukamilisha hatua ya robo leo asubuhi kuchezwa michezo minne mapema asubuhi ilipigwa mbungi kali kati ya walima michicha wa JKU dhidi ya wafanya biashara wa chukwani ICPS , ambapo dakika 90 za uwanjani walimaliza kwa sare ya goli moja kwa moja na kwenda hatua ya changamoto ya mikwaju ya penalty ambapo JKU wakipoteza mikwaju miwili na ICPS wakiweka kambani yote. Mchezo mwengine ikuwa kati ya maustadhi wa Almubarak almazruwi waliokuwa na kibarua kizito kwa wafanya biashara wa kisima majongoo Zanzibar Commercial, hiyo ikiwa ni kwa michezo ya saa mbili. Michezo ya saa nne izikutanisha Microtech waliopata ushindi rahisi mbele ya warembo wa miembeni Green Woman wa magoli matatu bila, huku waandaaji wa vyakula na vinywaji Mkokotoni wakikaribishwa kwenye vivutio vya utalii na watembeza watalii wa Amani ZOI kwa misumari miwili ya jahazi bila majibu. Kesho ligi hiyo itaendelea...