Michezo inawajenga kiakili wanafunzi na wazee wao.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, amewataka walimu na wazazi kushirikiana katika kukuza na kulea vipaji vya wanafunzi.

Hayo ameyaeleza wakati akifunga   Tamasha la tatu la Michezo la Skuli ya Leera la mwaka 2024 lililofanyika  kwenye uwanja wa Amani Complex .

Alisema watoto hao watakapoekewa mashirikiano baina pande zone mbili watakuja peperusha bendera ya Taifa katika kuimarisha michezo.

Aliwataka skuli ya Leera kuendelea kuibua vipaji kwani miundo mbinu ya michezo inaendelea kukua kwa kasi zaidi pia ni vyema kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa jitihada za kuimarisha sekta ya Michezo nchini.


Waziri Tabia alieleza Serikali imetenga fedha billion 70 katika sekta ya michezo, hivyo hawanabudi kuthamini michezo na kuiendeleza katika skuli kwa watoto wao.

Akisoma risala ya Skuli hiyo  Mkuu  wa  Utawala Jonathan Kahatano, alisema skuli hiyo inatoa taaluma bora ikiambatana na kuibua vipaji mbali mbali vya kitaaluma na kimichezo.

Alisema matarajio yao kufanya Tamasha la michezo kila mwaka ili  kuendelea kutoa fursa kwa wanafunzi wao kukuza  vipaji. 

" kama ujuavyo katika ulimwengu wa leo michezo ni ajira hivyo tunawapa nafasi wanafunzi ya kukuza vipaji vyao, kwani   wanaitaji utimamu wa mwili ili kuweza kufanya vizuri kitaaluma" alisema

Aidha alimuomba Waziri Tabia kila afanyavyo mipango ya wizara ya kimaendeleo ya michezo kuweza kuikumbuka skuli hiyo kwa lengo la kuimarisha michezo na vipaji kwa wanafunzi.

Zaidi ya michezo 50 imeshindaniwa wanafunzi  wa Primary, Nursery, Secondary kwa michezo mbali mbali.

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU