Historia ya Majestic cinema.
Historia Ya Majestic Cinema Na Kuunguwa Moto.
Majestic Cinema, iliyofunguliwa mnamo Oktoba 20, 1955, baada ya jengo la kwanza la sinema kuunguwa, ilikuwa ni fahari ya Zanzibar, Ilibuniwa na mbunifu maarufu Mzanzibari Dayalji Pitamber Sachania, baada ya sinema ya awali, Royal Cinema iliyojengwa 1921, kuteketea kwa moto mnamo Februari 8, 1954 ,siku hiyo kulikuwa na Zanana show ,ingawa nje kulikuwa na mabarobaro tele wakitia macho nuru, siku ambayo ikiendeshwa filamu inayoitwa Albela.Albela ni filamu ya vichekesho na muziki ya Bollywood ya 1951 iliyoongozwa na nyota Bhagwan Dada na Geeta Bali. Sinema Yakihindi ilikuwa ya kwanza kwa mapato ya juu kwa wakati huo na sinema ilijaa wanawake ikaleta mtafaruku mkubwa . Royal Cinema, iliyokuwa sinema ya kwanza ya kifahari katika Afrika Mashariki, ilifunguliwa na Hassanali Adamjee Jariwalla na kubuniwa na J.H. Sinclair,
Majestic Cinema ilikuwa na muundo mpya wa kipekee wa vishubaka vya mistari, na alama ya ndege flamingo, ikijumuisha skrini pana (cinemascope) ,mfumo wa sauti wa stereophonic na ilikuwa na technicolor. Iliweza kutoa nafasi kwa watu 900 na ushey, ikiwa na balcony kubwa . Tiket zikiuzwa na Aghuli mara nyengine kulikuwa kuna kibiru watu wakigombania tiketi au ununue black maket (magendo) .Kulikuwa na mabodi skuli ya Vikokotoni yakitangaza kwa ajili ya sinema zote tatu nazo ni Royal Cinema ambayo ilojengwa 1921, Emper Cinema mwaka 1939 na Sultana (Cine Afrique Malindi ) iliyofunguliwa mwaka 1951,au nje kila sinema iliweka bodi lake . Pia kulikuwa mtu marufu akitwa Chepe ,ambae akibeba bodi la sinema (billboards) akitangaza mitaani, akipiga na kengele ,akihanikiza huanza (mfano) : Tarana itakuwa saa 12 jioni na saa 3 usiku , ijumamosi afternoon show saa 9.Ijumapili morning show saa 4 .ijumatatu Zanana show saa 9 au ladies show :.Chepe hutangaza kwa kukoleza husema :ngumi kama njugu- bisi, au one shilling all round : kulikuwa kukionyeshwa filamu za Kihindi,Kiarabu (Misri) na Kizungu .Jengo hilo lilikuwa na matumizi mengi zaidi, ikiwa ni pamoja na bar kwa wenye leseni tu,arimradi ilijengwa kama pahala pa kustarehe , mgahawa, kantini ya kuuza vitafunio,hoteli itwayo Pigalle baadae , ofisi za Air Tanzania, ikiuza tiketi, mkahawa mdogo na ofisi ya Chuo Kikuu cha Zanzibar. Abdullhussein Marashi, ambaye amekuwa akifanya kazi katika Majestic Cinema tangu mwaka wa 1982, anaendelea na urithi wa familia yake kwa kuhakikisha sinema hiyo inabaki kuwa endelevu. Jengo hilo kutakumbukwa kwa watu watano nao maarufu nao ni Dayalji ,Aghuli,Golo, Chepe na Khadija Abdillah .
Comments
Post a Comment