Posts

WANAFUNZI WAMEASWA KUENDELEA NA KIADATO CHA TANAO NA SITA KWENYE ELIMU YA SEKONDARI ILI KUEPUKA USUMBUFU UNAOWEZA KUJA KUWAKUTA HAPO BAADAE WATAKAPOTAKIWA KUTHIBITISHWA NA MAMLAKA ZA ELIMU YA JUU TANZANIA HAYO YAMEELEZWA NA MKURUGENZI WA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR NDUGU   IDDI KHAMISI  KATIKA MAHAFALI YA THELATHINI NA MOJA YA SHULE YA SEKONDARI YA NYUKI TPDF YALIYOFANYIKA SHULENI KWAO MWANAKWEREKWE MJINI UNGUJA NDUGU IDDI KHAMIS AMEWAASA WAZAZI NA WANAFUNZI KUFUATA UTARATIBU WA KIDATO CHA TANO NA SITA KWANI NDIO UNAOTAMBULIWA NA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NA KUACHA KUTUMIA NJIA ZA MKATO ZA KUTOKA KIDATO CHA NNE KWENDA DIGIRII HAUKUBALIKI NAE MKURUGENZI WA IDARA YA ELIMU YA SEKONDARI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR BI ASIA IDI ISSA AMEWATAKA WANAFUNZI KUTUMIA KIPINDI HICHO CHA KUSUBIRIA MATOKEO KUJISOMEA MASOMO YA KOMPUTER,KOZI ZA KIINGEREZA NA LUGHA NYENGINE ILI KUWAJENGEA MISINGI YA ELIMU MBELE WANAKO ELEKEA AKITOA NENO LA SHUKRANI MWALIMU ...
Image
FORO FORO FURAHA AU MISIBA? NA : HAMAI VUAI USSI Kama ambavyo wageni (sikusudii wa Bara) wanapo ingia Zanzibar aghalab hukusudia kuutembelea (mji mkongwe, sehemu za makumbusho hata za mashamba, kuona hali ya maisha ya watu kiujumla), na mwishowe kujimwaga Foro. Wageni wa nchi jirani wanapo ingia Z'bar, pia nao hukusudia matembezi ya sehemu za mji wa Zanzibar, na hatimae ni Foro. Amma sisi wenyewe Wazenj, kilele cha furaha yetu kuishi Z'bar, ni kuwepo Forodhani, kukoga, kutembea, kupiga soga, pia ndio meeting point ya wengi. Zanzibar bila ya Foro haipo. Tokea hapo kale, kukoga Forodhani au kujifundisha kukoga kwa styles zote huanzia au huishia hapo, Generation kwa generations. Kama ni hivo, Jee, municipal au serikali kwa jumla, imewahi kufikiria umuhimu wa eneo wanalokoga vijana wetu (usalama wake na unadhifu wake)? Jee hii sehemu muhimu ya bahari ambayo ni ukingo wa MAWE na ufukwe wa mawe - kokoto na machupa, tuseme serikali haioni au anatafutwa Mfadhili k...

PATA KUJUA ALICHOKIANDIKA NYALANDU

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa. AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA. VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna n...

kikosi cha wachezaji wa kike kutoka jumbi SAUTI SPORTS LADY

Image

VIJANA WA KIZANZIBAR WAKIONESHA UWEZO BINAFSI UWANJANI

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

Image
KWA WAPENZI WA SOKA VISIWANI ZANZIBAR SIKU YA JUMANNE VISIWA VITASIMAMA KWA DAKIKA KADHAA KUPISHA MECHI YA TIMU MBILI KALI KATI YA MIEMBENI CITY VS KMC AMBAZO KILA MOJA INAFAANYA MAANDALIZI KUELEKEA KUANZA LIGI. IKUMBUKWE KWA KMC HIYO ITAKUWA MECHI YAKE YA MWISHO YA KIRAFIKI VISIWANI ZANZIBAR IMESHACHEZA MECHI TANO NA KUSHINDA ZOTE SASA JE MIEMBENI CITY WATAWEZA KUVUNJA RECORD HIYO? WAKATI MIEMBENI CITY ISHACHEZA MICHEZO MITATU IKI SULUHU MMOJA NA KUSHINDA MICHEZO MIWILI   TIMU YA MANISPAA YA KINONDONI AMBAYO INANOLEWA NA KOCHA MAARUFU TANZANIA FRED FELIX MINZIRO AMBAE AMESHAWAHI KUFUNDISHA TIMU YA YANGA,JKT RUVU,SINGIDA UNITED AMBAYO MARA BAADA YA KUIPANDISHA DARAJA AKAHAMA NA KUHAMIA TIMU HIYO YA MANISPAA YA KINONDONI                                               FRED FELIX MINZIRO KWA MARA YA KWANZA ATASHUKA UWANJANI KIUNGO MATATA WA MIEMB...

CHINA BADO INAHITAJI USHIRIKIANO WA KIELIMU NA KIUTAMADUNI NA ZANZIBAR

Image
USHIRIKIANO katika Sekta ya Elimu na Utamaduni kati ya China na Zanzibar umeelezwa kuwa umesaidia sana katika kuendeleza urafiki baina ya wananchi wa nchi hizo mbili. Balozi  mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiao Wu alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  katika Ubalozi  wao  uliopo Mazizini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Walimu Nchini China. Alisema utamaduni wa China na Tanzania unafanana na wananchi wa nchi hizo mbili wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbali mbali ikiwemo biashara na makampuni ya China kuaminika katika kujenga Ofisi za Serikali na watu binafsi. Balozi Xie  alisisitiza kuwa  China itaendelea kuisaidia Tanzania  katika harakati zake za kiuchumi na hivi sasa wanasimamia ujenzi wa viwanja viwili vya michezo Mao tse tung na  wanatarajia kujenga bandari mpya katika eneo la Mpigaduri Mjini Zanzibar. Aliwapongeza vijna wa Zanzibar kwa kuwa na mwamko wa kujifunza lugha ya kichina katika Chuo K...