FORO
FORO FURAHA AU MISIBA?
NA : HAMAI VUAI USSI
Kama ambavyo wageni (sikusudii wa Bara) wanapo ingia Zanzibar aghalab hukusudia kuutembelea (mji mkongwe, sehemu za makumbusho hata za mashamba, kuona hali ya maisha ya watu kiujumla), na mwishowe kujimwaga Foro.

Wageni wa nchi jirani wanapo ingia Z'bar, pia nao hukusudia matembezi ya sehemu za mji wa Zanzibar, na hatimae ni Foro.

Amma sisi wenyewe Wazenj, kilele cha furaha yetu kuishi Z'bar, ni kuwepo Forodhani, kukoga, kutembea, kupiga soga, pia ndio meeting point ya wengi. Zanzibar bila ya Foro haipo.


Tokea hapo kale, kukoga Forodhani au kujifundisha kukoga kwa styles zote huanzia au huishia hapo, Generation kwa generations. Kama ni hivo, Jee, municipal au serikali kwa jumla, imewahi kufikiria umuhimu wa eneo wanalokoga vijana wetu (usalama wake na unadhifu wake)? Jee hii sehemu muhimu ya bahari ambayo ni ukingo wa MAWE na ufukwe wa mawe - kokoto na machupa, tuseme serikali haioni au anatafutwa Mfadhili kusafisha? Jee, hii nchi haina wahusika?

Foro, haupiti muda bila kupoteza maisha ya vijana wetu. Nani hajui hili? Hata hizi sehemu za vikuta vya kupumzikia, hazina kinga yeyote ya kutoanguka baharini. Maisha yote ya hapa petu ni kubahartisha tu kama maisha ya PAA msitu wa simba.

Lakini, na Forodha ya Wete Pemba, imekua kawaida kwamba kila mwaka lazima muhanga wa roho ya mtu. Kisa na sababu naamini ni uzembe wa wahusika kutoshughulika na maeneo haya.

SIJUI ITAKUA BORA KUPEWA WAGENI KUSHUGHULIKIA ?

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU