WANAFUNZI WAMEASWA KUENDELEA NA KIADATO CHA TANAO NA SITA KWENYE ELIMU YA SEKONDARI ILI KUEPUKA USUMBUFU UNAOWEZA KUJA KUWAKUTA HAPO BAADAE WATAKAPOTAKIWA KUTHIBITISHWA NA MAMLAKA ZA ELIMU YA JUU TANZANIA
HAYO YAMEELEZWA NA MKURUGENZI WA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR NDUGU  IDDI KHAMISI  KATIKA MAHAFALI YA THELATHINI NA MOJA YA SHULE YA SEKONDARI YA NYUKI TPDF YALIYOFANYIKA SHULENI KWAO MWANAKWEREKWE MJINI UNGUJA
NDUGU IDDI KHAMIS AMEWAASA WAZAZI NA WANAFUNZI KUFUATA UTARATIBU WA KIDATO CHA TANO NA SITA KWANI NDIO UNAOTAMBULIWA NA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NA KUACHA KUTUMIA NJIA ZA MKATO ZA KUTOKA KIDATO CHA NNE KWENDA DIGIRII HAUKUBALIKI
NAE MKURUGENZI WA IDARA YA ELIMU YA SEKONDARI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR BI ASIA IDI ISSA AMEWATAKA WANAFUNZI KUTUMIA KIPINDI HICHO CHA KUSUBIRIA MATOKEO KUJISOMEA MASOMO YA KOMPUTER,KOZI ZA KIINGEREZA NA LUGHA NYENGINE ILI KUWAJENGEA MISINGI YA ELIMU MBELE WANAKO ELEKEA
AKITOA NENO LA SHUKRANI MWALIMU MKUU WA SKULI HIYO LUTENI KHAMIS LUSUNA AMEWASHUKURU VIONGOZI WALIOHUDHURIA KATIKA HAFLA HIYO NA KUWAATAKA WANAFUNZI WAJIEPUSHE NA VISHAWISHI AMBAVYO VINAWEZA KUWAINGIZA KATIKA MAJARIBU
WAKISOMA RISALA YA WAHITIMU WA KIDATU CHA NNE WANAFUNZI FATMA MAZIGE NA GHANIA KHAMIS WAMESEMA KUTOKANA NA MAFANIKIO WALIYOYAPATA SHULENI HAPO NI PAMOJA NA KUTOA MCHANGO MKUBWA WA WACHEZAJI WA TIMU KUBWA NA KITAALUMA
PIA WAKITUMIA RISALA HIYO KUBAINISHA BAADHI YA CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SHULE HIYO AMBAZO NIPAMOJA NA UFINYU WA MAABARA,UPUNGUFU WA VYUMBA VYA KUSOMEA UKOSEFU WA WATAALAMU WA AFYA NK.

 KATIKA MAHAFALI HAYO MGENI RASMI ALIKUWA NI LUTENI KANALI  MUHAMMED SULEIMAN ALI MKUU WA HUDUMA YA KAMBI YA MTONI 

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU