Wizara ya afya Zanzibar kwa kushirikian na taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION wameendesha kambi ya matibabu ya midomo wazi katika hospitali ya mkoa Lumumba ikiwa ni muendelezo wa kambi zinazofanywa na taasisi hio ili kuhakikisha watoto wenye tatizo la midomo wazi wanapatiwa matibabu. Akizungumza katika kambi hio Mkurugenzi na muazilishi wa Taasisi hio Dr Piter Mabula amesema takriban miaka kumi na moja taasisi hio imekua ikitoa huduma hio na imefanikiwa kufanya matibabu wa watu zaid ya 2500 kwa Tanzania bara na visiwani ambapo kwa zanzibbar zaid ya watu 200 wamepatiwa huduma hio Dr Piter Mabula Mkurugenzi wa taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION Kwa upande wake Dr Sumaiya Said Abud kutoka katika hospitali ya mkoa Lumumba amesema kambi hio ya siku tano inatarajia kufanya matibabu ya watoto 25 ambao tayar watoto hao wamefanyiwa uchunguzi wa awali Dr Sumaiya Said Abud hospitali ya mkoa Lumumba Sambamba na hayo sumaiya ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye...
Posts
Mshike mshike wa Polisi Jamii Cup magharibi B
- Get link
- X
- Other Apps
MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP WILAYA MAGHARIBI B YALIENDELEA TENA KWENYE VIWANJA VIWILI TOFAUTI.KWENYE DIMBA LA KIEMBE SAMAKI KULIKUWA NA PAMBANO KATI YA NYAMANZI CITY NA CHUNGA CITY MATOKEO IKIWA NI GOLI 4 KWA 1 MAGOLI YA CHUNGA YALIFUNGWA NA YASSIR MOHD DAKIKA YA 7 NA GOLI LA PILI LILIFUNGWA TENA NA YASSIR MOHD DAKIKA YA 12. NA BAO LA KUFUTIA MACHOZI LA NYAMANZI CITY LIMEFUNGWA DAKIKA YA 39 NYAMANZI WALIPATA BAO LA KUFUTIA MACHOZI LILILOFUNGWA NA JUMA KOTO .DAKIKA YA 68 SAID SALUM ALIPATIA TENA CHUNGA CITY BAO LA TATU NA DAKIKA YA78 EVEREST ALIPATIA CHUNGA CITY GOLI LA NNE. KWENYE MCHEZO HUO MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP NA MKUU WA KITUO CHA POLISI MAZIZINI SP- SALUM NGAYANA ALIMKABIDHI MPIRA YASSIR MOHD KWA KUWA MAN OF THE MATCH ALIPATIA MABAO MAWILI NA ASSIST MBILI . KULE DIMBA LA NGOME KULIKUWA NA MPAMBANO KATI YA SHUBA SHUBA FC NA KOMBENI FC MATOKEO NI KOMBENI FC WAMESHINDA KWA PENATI 5 KWA 4 DHIDI YA SHUBA SHU...
KMKM yaondoka na alama tatu kibindoni kio
- Get link
- X
- Other Apps
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo kocha msaidizi wa Ibrahim Khamis Khatib amesema wapinzani wao walikuja kwa kupania mchezo ndio kilichowafanya washinde magoli wawili. Amesema mchazaji samir ametoka kwenye majeraha ndio maana hayukp vizuri. Ibrahim amewataka washabiki wa KMKM kuja viwanjani kuona kandanda inavyochezwa. Nae kocha wa muembe makumbi Rajab Mrisho amesema waamuzi bado wana mapungufu ndio maana wamepoteza mchezo wa leo. Amesema mchezo ulianza vizuri kipindi cha kwanza mabadiliko yamekuja kipindi cha pili amedai licha ya mchezo kwenda nao vizuri, wachezaji wake wamejituma wakishindwa kwenye mipango na kupelekea kufungwa goli mbili kwa moja.
Historia ya Majestic cinema.
- Get link
- X
- Other Apps
Historia Ya Majestic Cinema Na Kuunguwa Moto. Majestic Cinema, iliyofunguliwa mnamo Oktoba 20, 1955, baada ya jengo la kwanza la sinema kuunguwa, ilikuwa ni fahari ya Zanzibar, Ilibuniwa na mbunifu maarufu Mzanzibari Dayalji Pitamber Sachania, baada ya sinema ya awali, Royal Cinema iliyojengwa 1921, kuteketea kwa moto mnamo Februari 8, 1954 ,siku hiyo kulikuwa na Zanana show ,ingawa nje kulikuwa na mabarobaro tele wakitia macho nuru, siku ambayo ikiendeshwa filamu inayoitwa Albela.Albela ni filamu ya vichekesho na muziki ya Bollywood ya 1951 iliyoongozwa na nyota Bhagwan Dada na Geeta Bali. Sinema Yakihindi ilikuwa ya kwanza kwa mapato ya juu kwa wakati huo na sinema ilijaa wanawake ikaleta mtafaruku mkubwa . Royal Cinema, iliyokuwa sinema ya kwanza ya kifahari katika Afrika Mashariki, ilifunguliwa na Hassanali Adamjee Jariwalla na kubuniwa na J.H. Sinclair, Majestic Cinema ilikuwa na muundo mpya wa kipekee wa vishubaka vya mis...
Photo from Ali Ghullam
- Get link
- X
- Other Apps
Petroleum imepanda kwa shilling mia moja na mbili kwa bei mpya ya mwezi wa tisa, ambapo bei ya awali ilikua ni 3063 , wakati bei ya diesel imeshuka kwa shilling kumi na mbili ambapo awali ilikua ikiuzwa kwa shilling 3259 na bei ya mafuta ya taa ikibaki kawa ilivyo haikuongezeka wala kupanda. Bei ya mafuta ya ndege yakushuka kwa shillings sita ambapo yalikuwa yakiuzwa kwa shs 2843. Hii imetokana na taarifa zinazo tolewa na mamlaka ya maji na nishati Zanzibar ZURA leo tarehe 8 September 2024 huko ofisini kwao maisara mjini Unguja.
KUELEKEA MCHEZO WA MUEMBE MAKUMBI NA NEW CITY TAMBO HIZI APA.
- Get link
- X
- Other Apps
Michezo inawajenga kiakili wanafunzi na wazee wao.
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, amewataka walimu na wazazi kushirikiana katika kukuza na kulea vipaji vya wanafunzi. Hayo ameyaeleza wakati akifunga Tamasha la tatu la Michezo la Skuli ya Leera la mwaka 2024 lililofanyika kwenye uwanja wa Amani Complex . Alisema watoto hao watakapoekewa mashirikiano baina pande zone mbili watakuja peperusha bendera ya Taifa katika kuimarisha michezo. Aliwataka skuli ya Leera kuendelea kuibua vipaji kwani miundo mbinu ya michezo inaendelea kukua kwa kasi zaidi pia ni vyema kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa jitihada za kuimarisha sekta ya Michezo nchini. Waziri Tabia alieleza Serikali imetenga fedha billion 70 katika sekta ya michezo, hivyo hawanabudi kuthamini michezo na kuiendeleza katika skuli kwa watoto wao. Akisoma risala ya Skuli hiyo Mkuu wa Utawala Jonathan Kahatano, alisema skuli hiyo inatoa taaluma bora ikiambatana ...
ALMUBARAK na ZOI wakubali kuwa madaraja ya fainali.
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya kukubali kipigo cha goli moja bila chuo cha Almubarak almazruwi kutoka kwa Mafundi umeme wa magomeni makada chuo cha Microtech kesho wata , jitupa uwanjani kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya watembeza watalii wa Amani ZOI language waliofanywa daraja na chuo cha Microtech kwa kutandikwa bakora mbili bila majibu. Kesho asubuhi ZOI na Almubarak watacheza kujua nafasi ya tatu na ya nne. Mchezo wa fainali utapigwa Mao ze Dong siku ya Jumapili hii ikiwakutanisha ICPS wakiumana na Microtech.
WALIWOONGOZA KWENYE MAKUNDI WAKWAMA KWA NAMBA NNE.
- Get link
- X
- Other Apps
Mashindano ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo na vituo vya mafunzo ya amali yameingia hatua ya nusu fainali baada ya kukamilisha hatua ya robo leo asubuhi kuchezwa michezo minne mapema asubuhi ilipigwa mbungi kali kati ya walima michicha wa JKU dhidi ya wafanya biashara wa chukwani ICPS , ambapo dakika 90 za uwanjani walimaliza kwa sare ya goli moja kwa moja na kwenda hatua ya changamoto ya mikwaju ya penalty ambapo JKU wakipoteza mikwaju miwili na ICPS wakiweka kambani yote. Mchezo mwengine ikuwa kati ya maustadhi wa Almubarak almazruwi waliokuwa na kibarua kizito kwa wafanya biashara wa kisima majongoo Zanzibar Commercial, hiyo ikiwa ni kwa michezo ya saa mbili. Michezo ya saa nne izikutanisha Microtech waliopata ushindi rahisi mbele ya warembo wa miembeni Green Woman wa magoli matatu bila, huku waandaaji wa vyakula na vinywaji Mkokotoni wakikaribishwa kwenye vivutio vya utalii na watembeza watalii wa Amani ZOI kwa misumari miwili ya jahazi bila majibu. Kesho ligi hiyo itaendelea...
Makunduchi, INCLUSIVE,za bwagwa robo fainali mashindano ya VTA.
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya kukamilisha hatua ya makundi ligi ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali leo timu nane 8 zatinga robo fainali ZOI language ikikamilisha idadi hiyo baada ya ushindi wa goli mbili bila dhidi ya watafsiri maneno kwenda ishara chuo cha Inclusive kwenye mchezo wa kiporo kilicho wanufaisha ZOI. Timu ya Makunduchi, Inclusive na Mwanakwerekwe zikimaliza hatua ya makundi kwenye kundi A. Na upande wa kundi B chuo cha ZAWA, DHOW Country na chuo cha Mwenge wote wakiishia safari yao hapo wakiwaavha mafahali waendelee na vita hapo kesho katika hatua ya robo fainali. Vyuo hivyo ni Zanzibar Commercial atakipiga dhidi ya Almubarak, JKU atapigishana kwata na ICPS, ZOI wakijaribu bahati yao kwa wahudumu wa hotelini Mkokotoni, huku Microtech wanawsalika warembo wa miembeni Green Woman.
JKU YAMALIZA MAKUNDI KWA KUWEKA HESHMA.
- Get link
- X
- Other Apps
Timu ya chuo cha ufundi JKU kimezima harakati za burudani kutoka mizingani forodhani kwa DHOW Country baada ya kuwaadabisha kwa bakora sita mtawalia katika mchezo wa mapema asubuhi ya leo. JKU walikuja kamili kuisaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi B ambapo katika kundi hilo yeye na Microtech ndio wanagombea nafasi hiyo. Wakati wapinzani wao DHOW Country walikuja pungufu na kuwafanya JKU wapate wepesi wa ushindi huo mkubwa. Michezo mengine ikiwakutnisha ZOI watembeza watalii wa Amani waliofungwa goli mbili kwa moja dhidi ya wafanya biashara wa kisima majongoo Zanzibar Commercial ambao bado wapo kileleni baada ya ushindi wa leo wakikusanya alama kumi na tatu 13 ambapo kwenye group lao hakuna atae fikisha. Chuo cha Almubarak almazruwi wakikubali kipigo cha goli moja kwa nunge dhidi ya Watoa huduma hotelini Mkokotoni, mchezo wa mwisho ikiwakutanisha ndugu wawili kati ya Mwanakwerekwe dhidi ya Makunduchi, ambapo wote wakiweka tegemeo la adui muombee njaa ili wapate nafasi ya kutin...
Microtech na Green Woman wakata tiketi ya Robo fainali.
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya kukamilisha michezo 6 sita ya kundi B chuo cha Microtech wamekata tiketi ya Robo fainali ya michuano ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali baada ya ushindi wa goli moja kwa nunge dhidi ya watoa huduma hotelini Mkokotoni na kuwasafirisha hadi nafasi ya kwanza wakisubiri hatma ya kubakia hapo baada ya mchezo wa mwisho wa JKU. Warembo wa miembeni Green Woman nao tayari wamekata tiketi hiyo ya robo fainali baada ya kukamilisha michezo 6 sita ya kundi A na kuondoka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya watafsiri maneno kutoka mombasasa Inclusive ambao bado wapo kwenye mabano kutinga robo fainali ya kundi hilo, timu nyengine iliyokamilisha michezo 6 sita ni ICPS wenye alama 9 tisa, Green Woman wameungana na Zanzibar Commercial wenye alama 10 licha ya kipigo cha leo kutoka kwa ICPS cha goli mbili bila. Michezo mengine ni Maustadhi wa Almubarak almazruwi wakiwaadhibu wapiga za music DHOW Country goli mbili bila majibu.
Microtech yaramba shubiri ya wakulima wa mpunga JKU.
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya ushindi wa michezo minne mfululizo Microtech hatimae leo ameonja chungu ya jiwe baada ya kupokea kipigo cha paka mwizi kutoka kwa wakulima wa mpunga JKU cha misumari minne kwa moja katika mchezo wa mapema ulikuwa wa kutafuta nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi lao. Mchezo mwengine uliwakutanisha wacheza kibati kutoka Amani mkoa na Mafundi magari kutoka Mkokotoni ambapo karata zao hazikutoa mbabe na badala yake kugawana alama moja kwa sare tasa ya sifuri bin sifuri. Michezo mengine ya saa nne ikiwakutnisha ZOI watembeza watalii wa Amani dhidi ya wafanya biashara wa chukwani ICPS kwa kutoka suluhu ya goli 2 mbili kwa mbili, mchezo uliochezwa kwa tahadhari kubwa kila upande Mchezo wa mwisho ulionesha mpira kukosa huruma kwa jenenza la wavuvi wa tasi na pono wa Makunduchi kugongomelewa msumari wa moto na warembo wa miembeni Green Woman kwa kichapo cha goli moja kwa nunge. Mashindano hayo ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali yanaendelea tena kesho k...
Wavuvi wa tasi na pono Makunduchi wafia mikononi mwa watafsiri maneno.
- Get link
- X
- Other Apps
Jinamizi la matokeo mabaya kwa chuo cha Makunduchi waliobeba dhana ya uchumi wa buluu wakuwa na msimu mbaya tokea kuingia kwenye mashindano hayo. Katika mchezo wa leo Makunduchi walikuwa wanatafuta nafasi yakucheza robo fainali mambo hayakuwa mambo nakujikuta kwenye dema kuingia mwenyewe akipigwa rungu tatu kwa mbili zake dhidi ya watafsiri wa lugha Inclusive, wakati huo wapiga ala za music wakeshaji DHOW Country wakiwatolea machofu wacheza kibati Mwenge kwa misumari minne ya moto dhidi ya mbili zilizorejesha matumaini ya Mwenge kutaka kugomboa lakini wapiga mziki hao wakakaza nyuzi za Dumbak na kuondoka na alama tatu kibindoni, Maustadhi wa Almubarak almazruwi wakija kwa kujiamini baada ya kufuatilia michezo ya Waunga maji mitaani ZAWA na kuondoka na alama tatu kwa ushindi wa goli mbili kwa moja, washona nguo na Mbao Mwanakwerekwe wakifanya biashara ya suluhu na Zanzibar Commercial kwa sare tasa ya sifuri bin sifuri. Ligi hiyo itaendelea kesho kwa raundi ya saba 7 ,Mechi za kesho...
Mafundi umeme wa magomeni Kakada wawasha taa nyekundu.
- Get link
- X
- Other Apps
Ligi ya mpira wa miguu Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali ikiendelea kuipamba haiba ya viwanja vya Zanzibar yaendelea tena leo kwa michezo minne eo Jumanne ya tarehe 20 .08.2024. Warembo wa Miembeni matumbaku GREEN WOMEN wamewabana mbavu chuo cha ICPS kwa sare ya goli moja kwa moja 1-1 katika mchezo wa mapema, ambapo wachonga mbao wa Mwanakwerekwe wakiendeleza wimbi baya la kupoteza mbele ya watembeza watalii wa Amani ZOI kwa kukubali kipigo cha goli moja 1 bila majibu, Wakati Mafundi umeme wa magomeni makada MICROTECH wakiondokka na alama zote tatu kwa maustadhi wa mombasa Almubarak almazruwi Kwa ushindi mnono wa 4G4 Almubarak wakipata goli moja 1 la kufutia machizi mchezo wa mwisho leo mafahali wawili wakigaragara zizi moja kati ya wakulima wa mboga mboga JKU dhidi ya wapishi wa mboga hizo Mkokotoni wakiondokka na sare Tasa ta sifuri na kugawana alama moja moja. Kesho mashindano hayo yanaendelea kwa michezo minne Waunga m...