TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

Kuna khabari zinaenea mitandaoni juu ya kijana IDDI THABIT (IT). kuwa ameritadi na taarifa hizo kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kasi kubwa zikidai yakuwa IDDI ameritadi amezikanusha kauli hizo leo hii mchana wakati akifanyiwa mahojiano maalumu kwenye kipindi cha minus ten cha HITS FM RADIO 
Msanii mkongwe wa muziki wa Zenji Fleva,Iddi Thabit (I.T) ambaye pia alikuwa kiongozi wa nidhamu katika chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar.
IDDI amesema waliovumisha jambo hilo hawakuwa na nia njema kwake na walitaka kumuharibia jina lake mbele ya jamii ya kizanzibar na tanzania kiujumla.
Akiongea kwa masikitiko wakati akihojiwa na mtangazaji na DJ maarufu visiwani zanzibar SAID ABDALLA au kwa jina maarufu DJ SIDE amesema ingekuwa hayupo kwenye nchi hii angekuwa yupo nje ya Tanzania jamii ingeamini lakini kwa vile kila saa yupo mitaani imekuwa shida kidogo kuaminika uvumi huo.
hivyo basi IT amewataka wazanzibar kupuuza usemi huo na kumuombea dua mola wake amuepushe na ushetani huo kwani yeye bado ni muislamu safi.
nilipopita kwenye mitandao ya kijamii nika kutana na baadhi ya post ambazo zikitakia mema IDDI THABI (IT) mfano kama hizi:-

"Huyu ni msanii wa kizanzibari ambaye anaimba, sipendi nikitaje kile kinachosambaa kwamba amekifanya, lakini napenda niseme kama ni kweli ameamua hivyo basi namuombea kwa Mwenyezi Mungu (Allah) amkurupushe huko aliko akumbuke na amuombe msamaha mwenyezi Mungu,atubie toba ya kweli ili abaki salama hapa duniani na huko akhera ambako ndio mafikio yetu sote - Amiin.
Pamoja na dua hii, kwa kuwa hujafa hujaumbika pia Allah atunusuru sisi, watoto na vizazi veytu na maamuzi kama hayo ikiwa ni kweli IDDI THABIT (IT) ameyafanya au hata iwe hakufanya maamuzi hayo."

nyengine.....Salum Chopa  "Aslama alekum huyu jamaa nilikutana nae muda mfupi kazini na nilimuhoji kuhusu ana na tuhuma hizo lkn mwenyewe amekanusha habari hizo si kweli yeye ni muislamu halisi"


IDDI THABIT (I.T)

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU