BODI YA UWEZESHAJI WIZARA YA KAZI YATAKIWA KUWA WAAMINIFU.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto DR. Moudline Cyrus Castico ameitaka Bodi ya Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Ki uchumi kufanyakazi zake kwa ushirikiano ,uaminifu na kujituma ili Mfuko huo uwe endelevu . Hayo ameyaeleza wakati akizindua Bodi hiyo huko kwenye ukumbi wa Wizara yake Mwanakwerekwe wilaya ya Magharib B’ Unguja. Amesema kwa kufanya hivyo Mfuko huo utafikia malengo yake na kutoa huduma za Mikopo kwa Wajasiriamali na Wananchi kwa ujumla. Dr. Moudline amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha Mfuko huo ilii Wananchi wake wakopeshwe ili kutunisha fedha za miradi yao wanayoiendesha ili kuweza kujiajiri na kujipunguzia umaskini. “Mahitaji yamekua makubwa maombi ya Mikopo yanapokelewa kila siku ,hivyo mshirikiane na Uongozi wa Wizara ili kupata mbinu za pamoja za kutunisha fedha kupitia Mfuko huo “Ameisisitiza bodi hiyo . Halkadhalika ameitaka Bodi kujenga tabia ya k...