Chaneza Waanzisha mashindano mapya ili kuupa hamasa mchezo huo.
Mashindano
ya mpira wa pete kwa kuadhimisha moaka 55ya mapindizi ya Zanzibar yanatarajiwa kukata
utepe hapo kesho katika uwanja wa jimkana saa kumi za jioni timu nane za kike
zitashiriki mashindano hayo.
Akiongea na
kipindi hiki katibu mkuu wa chama cha mpira wa pete zanzibar Saidi Ali Mansab
amesema maandalizi kwa upande wao yamekamilika na kinachosubiriwa ni wakati na
filimbi kupuulizwa.
Amesema
mashindano hayo yamepewa baraka na kamati ya sherehe na mapambo kwa kuwawezesha
chama cha Netbal kuandaa mashindano hayo
Mashindano
ya Mapinduzi Cup kwa netball ni ya kwanza kufanyika hapa Zanzibar na kwa mujibu
wa katibu wa chaneza amesema wanatarajia kuwa endelevu ili kila mwaka yaweze
kufanyika kwani wana malengo makubwa ya baadae.
Comments
Post a Comment