MICHEZO MIDOGO INAANZA KUIMARISHWA KUPITIA SHAMRASHAMRA ZA SHEREHE ZA MAPINDUZI
Mchezaji Makame Juma
(Ronaldo) amefanikiwa kushinda kombe la Draft Mapinduzi Cup baada ya kumfunga
Azizi Abdallah (Ostadh) kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa
kwenye Maskani ya Stone Baret iliyopo Kibanda Maiti.
Akiyafunga Mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya
Kusini Unguja Idrissa Kitwana amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar ni kuinua michezo yote ili vijana wapate fursa mbali mbali kupitia
michezo.
Nae Mbunge wa Jimbo Shaurimoyo Mattar Ali
Salum ambae nae alishiriki Katika Mashindano hayo, amesema msimu ujao
wanatarajia kuyaboresha Mashindano hayo kwa kushirikisha wachezaji wengi kutoka
majimbo tofauti huku mshindi akitarajiwa kupewa zawadi ya Mbuzi Mnyama.
Mchezaji Aziz Abdallah ambae ameshindwa
kwenye fainali amezungumza na ZBC huku akisesema Mashindano hayo yalikuwa na
ushindani mkubwa ambapo amekiri mpinzani wake alimzidi kiwango.
Bingwa wa Mashindano hayo Makame Juma
(Ronaldo) amesema alijiandaa kushinda taji hilo ndio maana amefanikiwa kutwaa
kombe hilo.
Nae Ramadhan Abdallah (Manyama) ambae ni
mratibu wa mashindano hayo amesema wamejipanga kuhakikisha mwakani
wanayaboresha Mashindano hayo.
Jumla ya wachezaji 24 walishiriki
Mashindano ya Draft Mapinduzi CUP ambao waligawanywa kwenye makundi mawili A na
B huku kila kundi likijumuisha wachezaji 12 ambapo lengo la Mashindano hayo ni
kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyotokea January 12 mwaka 1964.
Comments
Post a Comment