UBINGWA NI WETU KWA VILE BADO TUNAUSHIKILIA WAMEJITAPA TIMU YA UHAMIAJI

NA:  Mwajuma Juma

MABINGWA watetezi wa Netiboli Tanzania timu ya Uhamiaji wanaondoka kesho kuelekea Mkoani Moshi kwa ajili ya kushiriki michuano ya klabu  Bingwa Tanzania.

Michuano hiyo ambayo inaanza Agosti 13-23 mwaka huu, ambapo Uhamiaji wakiwa mabingwa mara  mbili wamejipanga kuhakikisha wanatetea ubingwa wao huo.

Katibu wa michezo  wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Abrahman Karume ameliambia gazeti hili kuwa wanaondoka wakiwa na matumaini kibao ya kutetea ubingwa huo.

Alisema kuwa hilo kwao halina Shaka na kwa uimara wa timu yao anaimani watafanikisha malengo yao.

"Timu yangu naiamini na mwalimu amejitahidi kuifundisha ili iwe timu bora na inatia moyo wachezaji wote wanaonesha mwamko wa kutetea ubingwa huo", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kiujumla maandalizi yapo vizuri na wanakwenda huko kushindana na sio kushiriki.

" Maandalizi yapo vizuri na tumejipanga kiasi ya kwamba tunakwenda kutetea ubingwa wetu na imani tutashinda", alisema.

Hata hivyo alisema kuwa ni matumaini yake kuwa wanakwenda huko kwa ajili ya kupambana ili warudi na kombe na kutawazwa ubingwa kwa mara  ya tatu wa mashindano hayo.

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU