Posts

Showing posts from July, 2017

MIPIRA MIWILI YAONDOKA UWANJANI NA WACHEZAJI KWENYE MECHI MOJA

PROFESER RAI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU TEHAMA NCHINI

NA BIN GHULLAM. Ushirikiano baina ya vyuo vikuu vya nje na vyuo vikuu vya ndani kutawezesha wanafunzi kuwa na taaluma mzuri ya masomo ya Tehama ambayo imekuwa ndio mwenendo wa ulimwengu huu wa utandawazi huku akipigimifano ya nchi kama vile Ghana na Kenya ambao wamekuwa wakitengeneza program za mfumo wa computer ambao umeliteka soko kubwa la vijana. Kauli hiyo ametolewa na makamu mkuu wa chuo kikuu cha taifa Zanzibar Suza Pro. Idriss Ahmad Rai juu ya ujio wa wageni kutoka chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda. prof. Rai amesema kutokana na ulimwengu wa sayansi na Teknolojia, ushirikiano huo utawezesha walimu kutoka nchi mbali mbali kutoa mafunzo katika chuo cha Suza na kuwezesha kuwa na wataalamu wazuri katika fani mbali mbali ambazo zinatolewa hapa nchini. Pro. Rai amebainisha kuwa chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutoa program mbali mbali kwa lengo la kuleta ushindani katika soko la ajira ndani ya africa mashariki na dunia kiujumla. Aidha Por. Rai amesema pamo...

pata kujua kuhusu Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 23.07.2017 na kwengineko duniani

NA : BIN GHULLAM Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 80 kumtaka Philippe Coutinho, 25, kutoka Liverpool. (Sunday Mirror) Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, 30, ameiambia klabu yake kumsajili mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 23. (Don Balon) Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema Coutinho "ametulia" Liverpool baada ya klabu hiyo kuzungumza naye kufuatia hatua ya Barcelona kumtaka. (ESPN FC) Liverpool hatimaye wamefikia makubaliano na RB Leipzig ya pauni milioni 75 ili kumsajili Naby Keita. (Winner Sports) Meneja wa Arsenal amekanusha taarifa kuwa Alexis Sanchez, 28, anakaribia kuhamia Paris Saint-Germain kwa pauni milioni 70. (Standard) Alexis Sanchez anataka mshahara wa pauni 500,000 kwa wiki kutoka Paris Saint-Germain, huku akikaribia kuhamia Paris. (The Mirror) Liverpool na Arsenal wameonesha dalili za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Lucas Vasquez. (Diario Madridista) Chelsea wanapanga kuzungumza na Arsenal kuhusiana na Alex ...

Zanzibar yapoteza uanachama wake CAF

Zanzibar imepokonywa uanachama wake katika Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) miezi minne baada ya kukubaliwa kuwa mwanachama. Rais wa Caf Ahmad amesema Zanzibar, ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haikufaa kukubaliwa kuwa mwanachama wa 55 wa shirikisho hilo mwezi Machi. "Walipokelewa bila ya kufuatwa kwa sheria za shirikisho ambazo ziko wazi," amesema Ahmad. "Caf haiwezi kukubalia uanachama wa mashirikisho mawili kutoka kwa taifa moja." "Ufafanuzi wa maana ya taifa unatoka kwa Muungano wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa," amesema Ahmad katika mkutano mkuu wa kipekee wa shirikisho hilo nchini Morocco. Fifa ilikataa kuipokea Zanzibar kama mwanachama hata baada ya hatua ya Caf, iliyoidhinishwa na mtangulizi wa Ahmad, Issa Hayatou. Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini imekuwa ikiendesha shughuli zake za soka kivyake na kuwakilishwa katika mashindano ya soka ya kanda. Zanzibar imedumu kwa siku mia moja n...

FUATILIA Tetesi za soka Jumamosi 22-7-2017 KUTOKA DUNIANI

Tetesi za soka Jumamosi 22-7-2017 NA: BIN GHULLAM Mshambuliaji wa Barcelona Neymar mwenye umri wa miaka 25 amewaambia wachezaji wenzake kwamba atajiunga na Paris St-Germain huku klabu hiyo ya Ufaransa ikitaka kumnunua nyota huyo wa Brazil kwa kitita cha rekodi ya pauni milioni 196. (Le Parisen - in French) Lakini Meneja wa Barcelona Ernesto Valverde anasema kuwa habari zinazomuhisisha Neymar na PSG ni uvumi na kwamba wanamtaka kusalia (Metro) Mchezaji mwenza Javier Mascherano bado anafikiri kwamba klabu hiyo ya La liga inaweza kumzuia Neymar akisema kuwa ndio tegemeo la klabu hiyo siku zijazo.(ESPN FC) Barca inamlenga mshambuiliaji wa Argentina Paulo Dybala mwenye umri wa miaka 23 kutoka Juventus , iwapo Neymar ataondoka. (Mundo Deportivo - in Spanish) Manchester City imekubali kumnunua beki wa kushoto Benjamini Mendy kutoka Monaco kwa kitita cha pauni milioni 57(L'Equipe - in French) Tayari PSG imejitayarisha kuwasilisha ombi la kitita cha pauni milioni 70 kwa msham...

MKOA WA KUSINI UGUJA WAWEKA BAYANA MIKAKATI YA SEREKALI YA KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII

MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA DKT IDRISSA MUSLIM HIJJA  AMESEMA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ITAANZA KUZIHUSISHA SEKTA ZA ELIMU, AFYA NA KILIMO KWENYE BAJETI YA HALMASHAURI ZA WILAYA KWA AZMA YA KUSOGEZA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII KUANZIA MWAKA MPYA WA FEDHA 2017/2018. DKT IDRISSA AMETOA KAULI HIYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAKUU WA WILAYA , WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NA MAAFISA WA IDARA ZA SERIKALI ZA MKOA HUO WAKATI WA MAFUNZO ELEKEZI JUU YA MPANGO WA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI ZA MITAA YALIYOFANYIKA HUKO TUNGUU WILAYA YA KATI UNGUJA. AKITOA MAFUNZO HAYO MKUU WA MKOA HUYO AMEWATAKA VIONGOZI HAO KUIBUA NA KUIMARISHA HUDUMA HIZO BILA YA HOFU ILI JAMII IFAIDIKE NA MABADILIKO HAYO YANAYOANZIA JULAI MWAKA  2017 KWA KUZIWEZESHA FURSA NA CHANGAMOTO ZA KIJAMII KUTOKA KATIKA SEKTA YA AFYA, ELIMU NA KILIMO KUANZWA KUTEKELEZWA KATIKA NGAZI ZA CHINI ILI ZIPATIWE UFUMBUZI KWA WAKATI BILA YA KUJITOKEZA ATHARI YOYOTE. WAKIELEZA MATUMAINI YAO VIONGOZI WA MKOA HUO WAMESEMA W...