FUATILIA Tetesi za soka Jumamosi 22-7-2017 KUTOKA DUNIANI

Tetesi za soka Jumamosi 22-7-2017
NA: BIN GHULLAM
Mshambuliaji wa Barcelona Neymar mwenye umri wa miaka 25 amewaambia wachezaji wenzake kwamba atajiunga na Paris St-Germain huku klabu hiyo ya Ufaransa ikitaka kumnunua nyota huyo wa Brazil kwa kitita cha rekodi ya pauni milioni 196. (Le Parisen - in French)
Lakini Meneja wa Barcelona Ernesto Valverde anasema kuwa habari zinazomuhisisha Neymar na PSG ni uvumi na kwamba wanamtaka kusalia (Metro)
Mchezaji mwenza Javier Mascherano bado anafikiri kwamba klabu hiyo ya La liga inaweza kumzuia Neymar akisema kuwa ndio tegemeo la klabu hiyo siku zijazo.(ESPN FC)
Barca inamlenga mshambuiliaji wa Argentina Paulo Dybala mwenye umri wa miaka 23 kutoka Juventus , iwapo Neymar ataondoka. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester City imekubali kumnunua beki wa kushoto Benjamini Mendy kutoka Monaco kwa kitita cha pauni milioni 57(L'Equipe - in French)
Tayari PSG imejitayarisha kuwasilisha ombi la kitita cha pauni milioni 70 kwa mshambuliaji wa Arsenal Alexi Sanchez mwenye umri wa miaka 28 na kumlipa mshahara wa £ 400,000 kwa wiki.(Daily Mirror)
Manchester United imewasilisha ombi la pauni milioni 35 kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea Nemanja Matic mwenye umri wa miaka 28 na wameambiwa kwamba wanaweza kumchukua kwa pauni milioni 50 (Daily Mirror)
Real Madrid wamekubaliana na Monaco na Kylian Mbappe kuhusu uhamisho utakaovunja rekodi ya pauni milioni 120 kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Sun)
Barcelona imemuonya kiungo wa kati wa Liverpool Phillipe Coutinho mwenye umri wa miaka 25 kwamba watamuandama mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele mwenye umri wa miaka 20 iwapo The Reds watakataa ombi lao. (Sun)
Arsenal wamepatiwa fursa ya kumsajili kiungo wa kati matata Rafinha mwenye umri wa miaka 24 kutoka Bercelona.(Sky Sports)
The Gunners pia wanakaribia kuingia mkataba na Crystal Palace ambao utapelekea beki Calum Chambers kuelekea katika uwanja wa Selhurst Park(Guardian)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anamtaka mshambiliaji wa Swansea Fernando Llorente kuwa kama mchezaji wa ziada wa Alvaro Morata lakini Swansea wanataka dau la pauni milioni 30 (Independent)
Mabingwa hao wa Uingereza pia wanamtaka kiungo wa kati Alex Oxlaide-Chamberlain na wanapanga mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.(Sky Sports)
Meneja Jurgen Klopp wa Liverpool anatarajiwa kumwambia kiungo wa kati Phillipe Coutinho kwamba hawezi kuondoka Liverpool kuelekea Barcelona , baada ya The Reds kukataa kitita cha pauni milioni 72(Times - subscription required)
Swansea ndio klabu ya hivi karibuni inayohusishwa na uhamisho wa thamani ya pauni milioni 20 wa kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere mwenye umri wa miaka 25(Daily Telegraph)

Meneja wa Marseille Rudi Garcia amethibitisha kuwa mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 30 hatajiunga na klabu hiyo.

Comments

michezo

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

KUELEKEA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI WAFAHAMU MABINGWA WA KOMBE HILO

Burudani ya mashindano ya Elimu bila malipo JKU na Makunduchi balaa.

TAARIFA ZA KURITADI KWA IDDI THABIT ( IT ) ZA KANUSHWA NA MWENYEWE

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU