MKOA WA KUSINI UGUJA WAWEKA BAYANA MIKAKATI YA SEREKALI YA KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII
MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA DKT IDRISSA MUSLIM HIJJA AMESEMA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
ITAANZA KUZIHUSISHA SEKTA ZA ELIMU, AFYA NA KILIMO KWENYE BAJETI YA HALMASHAURI
ZA WILAYA KWA AZMA YA KUSOGEZA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII KUANZIA MWAKA MPYA WA
FEDHA 2017/2018.
DKT IDRISSA AMETOA KAULI HIYO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAKUU WA
WILAYA , WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NA MAAFISA WA IDARA ZA SERIKALI ZA MKOA HUO
WAKATI WA MAFUNZO ELEKEZI JUU YA MPANGO WA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI ZA MITAA
YALIYOFANYIKA HUKO TUNGUU WILAYA YA KATI UNGUJA.
AKITOA MAFUNZO HAYO MKUU WA MKOA HUYO AMEWATAKA VIONGOZI HAO KUIBUA NA KUIMARISHA HUDUMA HIZO BILA
YA HOFU ILI JAMII IFAIDIKE NA MABADILIKO HAYO YANAYOANZIA JULAI MWAKA 2017 KWA
KUZIWEZESHA FURSA NA CHANGAMOTO ZA KIJAMII KUTOKA KATIKA SEKTA YA AFYA, ELIMU
NA KILIMO KUANZWA KUTEKELEZWA KATIKA NGAZI ZA CHINI ILI ZIPATIWE UFUMBUZI KWA
WAKATI BILA YA KUJITOKEZA ATHARI YOYOTE.
WAKIELEZA MATUMAINI YAO VIONGOZI WA MKOA HUO WAMESEMA
WANAAMINI KWAMBA MPANGO HUO UTAWANUFAISHA WANANCHI KATIKA KUANDAA MAZINGIRA BORA.
Comments
Post a Comment