PROFESER RAI AFUNGUKA MAZITO KUHUSU TEHAMA NCHINI
NA BIN GHULLAM.
Ushirikiano baina ya vyuo
vikuu vya nje na vyuo vikuu vya ndani kutawezesha wanafunzi kuwa na taaluma
mzuri ya masomo ya Tehama ambayo imekuwa ndio mwenendo wa ulimwengu huu wa utandawazi huku akipigimifano ya nchi kama vile Ghana na Kenya ambao wamekuwa wakitengeneza program za mfumo wa computer ambao umeliteka soko kubwa la vijana.
Kauli hiyo ametolewa na makamu
mkuu wa chuo kikuu cha taifa Zanzibar Suza Pro. Idriss
Ahmad Rai juu ya ujio wa wageni kutoka chuo kikuu cha Makerere nchini
Uganda.
prof. Rai amesema kutokana na
ulimwengu wa sayansi na Teknolojia, ushirikiano huo utawezesha walimu kutoka
nchi mbali mbali kutoa mafunzo katika chuo cha Suza na kuwezesha kuwa na
wataalamu wazuri katika fani mbali mbali ambazo zinatolewa hapa nchini.
Pro. Rai amebainisha kuwa chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutoa program
mbali mbali kwa lengo la kuleta ushindani katika soko la ajira ndani ya africa mashariki na dunia kiujumla.
Aidha Por. Rai amesema pamoja na ushirikiao mzuri uliopo
ni vyema wanafunzi kuongeza juhudi za kujisomea kupitia mitandao na kuacha kutumia matumizi yasiyo sahihi ili kuwajenga kimasomo na kukabiliana na soko la ajira kwenye visiwa vya zanzibar.
Comments
Post a Comment