baada ya haji manara kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya TFF makubwa yamemkuta HAJI SANDE MANARA.
Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba, Haji Manara.
Pamoja na kufungiwa mwaka mmoja, Manara amepigwa faini ya Sh milioni 9.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara amefanya utovu mkubwa wa nidhamu kwa uwongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na viongozi wake na ili kulinda heshma ya shirikisho hilo ndio wakapitia kwa kina matamshi aliyoyatoa manara na kubaini utovu wa nidhamu huo.
Comments
Post a Comment