Posts

PATA KUJUA ALICHOKIANDIKA NYALANDU

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa. AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA. VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna n...

kikosi cha wachezaji wa kike kutoka jumbi SAUTI SPORTS LADY

Image

VIJANA WA KIZANZIBAR WAKIONESHA UWEZO BINAFSI UWANJANI

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

Image
KWA WAPENZI WA SOKA VISIWANI ZANZIBAR SIKU YA JUMANNE VISIWA VITASIMAMA KWA DAKIKA KADHAA KUPISHA MECHI YA TIMU MBILI KALI KATI YA MIEMBENI CITY VS KMC AMBAZO KILA MOJA INAFAANYA MAANDALIZI KUELEKEA KUANZA LIGI. IKUMBUKWE KWA KMC HIYO ITAKUWA MECHI YAKE YA MWISHO YA KIRAFIKI VISIWANI ZANZIBAR IMESHACHEZA MECHI TANO NA KUSHINDA ZOTE SASA JE MIEMBENI CITY WATAWEZA KUVUNJA RECORD HIYO? WAKATI MIEMBENI CITY ISHACHEZA MICHEZO MITATU IKI SULUHU MMOJA NA KUSHINDA MICHEZO MIWILI   TIMU YA MANISPAA YA KINONDONI AMBAYO INANOLEWA NA KOCHA MAARUFU TANZANIA FRED FELIX MINZIRO AMBAE AMESHAWAHI KUFUNDISHA TIMU YA YANGA,JKT RUVU,SINGIDA UNITED AMBAYO MARA BAADA YA KUIPANDISHA DARAJA AKAHAMA NA KUHAMIA TIMU HIYO YA MANISPAA YA KINONDONI                                               FRED FELIX MINZIRO KWA MARA YA KWANZA ATASHUKA UWANJANI KIUNGO MATATA WA MIEMB...

CHINA BADO INAHITAJI USHIRIKIANO WA KIELIMU NA KIUTAMADUNI NA ZANZIBAR

Image
USHIRIKIANO katika Sekta ya Elimu na Utamaduni kati ya China na Zanzibar umeelezwa kuwa umesaidia sana katika kuendeleza urafiki baina ya wananchi wa nchi hizo mbili. Balozi  mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiao Wu alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  katika Ubalozi  wao  uliopo Mazizini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Walimu Nchini China. Alisema utamaduni wa China na Tanzania unafanana na wananchi wa nchi hizo mbili wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbali mbali ikiwemo biashara na makampuni ya China kuaminika katika kujenga Ofisi za Serikali na watu binafsi. Balozi Xie  alisisitiza kuwa  China itaendelea kuisaidia Tanzania  katika harakati zake za kiuchumi na hivi sasa wanasimamia ujenzi wa viwanja viwili vya michezo Mao tse tung na  wanatarajia kujenga bandari mpya katika eneo la Mpigaduri Mjini Zanzibar. Aliwapongeza vijna wa Zanzibar kwa kuwa na mwamko wa kujifunza lugha ya kichina katika Chuo K...

UBINGWA NI WETU KWA VILE BADO TUNAUSHIKILIA WAMEJITAPA TIMU YA UHAMIAJI

Image
NA:  Mwajuma Juma MABINGWA watetezi wa Netiboli Tanzania timu ya Uhamiaji wanaondoka kesho kuelekea Mkoani Moshi kwa ajili ya kushiriki michuano ya klabu  Bingwa Tanzania. Michuano hiyo ambayo inaanza Agosti 13-23 mwaka huu, ambapo Uhamiaji wakiwa mabingwa mara  mbili wamejipanga kuhakikisha wanatetea ubingwa wao huo. Katibu wa michezo  wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Abrahman Karume ameliambia gazeti hili kuwa wanaondoka wakiwa na matumaini kibao ya kutetea ubingwa huo. Alisema kuwa hilo kwao halina Shaka na kwa uimara wa timu yao anaimani watafanikisha malengo yao. "Timu yangu naiamini na mwalimu amejitahidi kuifundisha ili iwe timu bora na inatia moyo wachezaji wote wanaonesha mwamko wa kutetea ubingwa huo", alisema. Hata hivyo alisema kuwa kiujumla maandalizi yapo vizuri na wanakwenda huko kushindana na sio kushiriki. " Maandalizi yapo vizuri na tumejipanga kiasi ya kwamba tunakwenda kutetea ubingwa wetu na imani tutashinda", alisema. ...

UHAMIAJI WAPATA VIONGOZI WAPYA HUKU WAKIWEKA MATUMANI KWA MASHABIKI WAO

KLABU ya soka ya Uhamiaji imefanya uchaguzi na kumchaguwa Khamis Juma Ussi kuwa Mwenyekiti wao. Uchaguzi huo ambao ulifanyika juzi katika ofisi za timu hiyo Kilimani ulisimamiwa na Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Zanzibar ZFA wilaya ya Mjini  Juma Abdurabi ambae ndie aliekuwa Mwenyekiti wa uchaguzi huo akisaidiwa na katibu wake Yahya Juma Ali. Mbali na Mwenyekiti kuchaguliwa Ussi lakini pia wajumbe wa mkutano huo walimchaguwa Makame Issa Jecha kuwa Makamo Mwenyekiti. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Abdurabi alisema kuwa nafasi ya katibu ilichukuliwa na Saleh Abass nafasi ambayo awali nilikuwa ikishikiliwa na Abrahman Karume. Abass kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo atasaidiwa kazi  na Mwinyi Abdalla ambae amechaguliwa kuwa katibu Msaidizi wa timu hiyo. Viongozi wengine  waliochaguliwa ni Shaame Ali Hamad Mshika Fefha, Salum Iddi Ali Msaidizi Mshika Fedha na wajumbe watatu ni Ali Mang'aa, Malil Sultan na Nasra Juma Mohammed. Uongozi huo mpya uliochag...