Posts

MCHEZO WA KIRAFIIKI WASIMAMISHA VISIWA VYA ZANZIBAR KWA MASAA.

Image
KWA WAPENZI WA SOKA VISIWANI ZANZIBAR SIKU YA JUMANNE VISIWA VITASIMAMA KWA DAKIKA KADHAA KUPISHA MECHI YA TIMU MBILI KALI KATI YA MIEMBENI CITY VS KMC AMBAZO KILA MOJA INAFAANYA MAANDALIZI KUELEKEA KUANZA LIGI. IKUMBUKWE KWA KMC HIYO ITAKUWA MECHI YAKE YA MWISHO YA KIRAFIKI VISIWANI ZANZIBAR IMESHACHEZA MECHI TANO NA KUSHINDA ZOTE SASA JE MIEMBENI CITY WATAWEZA KUVUNJA RECORD HIYO? WAKATI MIEMBENI CITY ISHACHEZA MICHEZO MITATU IKI SULUHU MMOJA NA KUSHINDA MICHEZO MIWILI   TIMU YA MANISPAA YA KINONDONI AMBAYO INANOLEWA NA KOCHA MAARUFU TANZANIA FRED FELIX MINZIRO AMBAE AMESHAWAHI KUFUNDISHA TIMU YA YANGA,JKT RUVU,SINGIDA UNITED AMBAYO MARA BAADA YA KUIPANDISHA DARAJA AKAHAMA NA KUHAMIA TIMU HIYO YA MANISPAA YA KINONDONI                                               FRED FELIX MINZIRO KWA MARA YA KWANZA ATASHUKA UWANJANI KIUNGO MATATA WA MIEMB...

CHINA BADO INAHITAJI USHIRIKIANO WA KIELIMU NA KIUTAMADUNI NA ZANZIBAR

Image
USHIRIKIANO katika Sekta ya Elimu na Utamaduni kati ya China na Zanzibar umeelezwa kuwa umesaidia sana katika kuendeleza urafiki baina ya wananchi wa nchi hizo mbili. Balozi  mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiao Wu alieleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  katika Ubalozi  wao  uliopo Mazizini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Walimu Nchini China. Alisema utamaduni wa China na Tanzania unafanana na wananchi wa nchi hizo mbili wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbali mbali ikiwemo biashara na makampuni ya China kuaminika katika kujenga Ofisi za Serikali na watu binafsi. Balozi Xie  alisisitiza kuwa  China itaendelea kuisaidia Tanzania  katika harakati zake za kiuchumi na hivi sasa wanasimamia ujenzi wa viwanja viwili vya michezo Mao tse tung na  wanatarajia kujenga bandari mpya katika eneo la Mpigaduri Mjini Zanzibar. Aliwapongeza vijna wa Zanzibar kwa kuwa na mwamko wa kujifunza lugha ya kichina katika Chuo K...

UBINGWA NI WETU KWA VILE BADO TUNAUSHIKILIA WAMEJITAPA TIMU YA UHAMIAJI

Image
NA:  Mwajuma Juma MABINGWA watetezi wa Netiboli Tanzania timu ya Uhamiaji wanaondoka kesho kuelekea Mkoani Moshi kwa ajili ya kushiriki michuano ya klabu  Bingwa Tanzania. Michuano hiyo ambayo inaanza Agosti 13-23 mwaka huu, ambapo Uhamiaji wakiwa mabingwa mara  mbili wamejipanga kuhakikisha wanatetea ubingwa wao huo. Katibu wa michezo  wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Abrahman Karume ameliambia gazeti hili kuwa wanaondoka wakiwa na matumaini kibao ya kutetea ubingwa huo. Alisema kuwa hilo kwao halina Shaka na kwa uimara wa timu yao anaimani watafanikisha malengo yao. "Timu yangu naiamini na mwalimu amejitahidi kuifundisha ili iwe timu bora na inatia moyo wachezaji wote wanaonesha mwamko wa kutetea ubingwa huo", alisema. Hata hivyo alisema kuwa kiujumla maandalizi yapo vizuri na wanakwenda huko kushindana na sio kushiriki. " Maandalizi yapo vizuri na tumejipanga kiasi ya kwamba tunakwenda kutetea ubingwa wetu na imani tutashinda", alisema. ...

UHAMIAJI WAPATA VIONGOZI WAPYA HUKU WAKIWEKA MATUMANI KWA MASHABIKI WAO

KLABU ya soka ya Uhamiaji imefanya uchaguzi na kumchaguwa Khamis Juma Ussi kuwa Mwenyekiti wao. Uchaguzi huo ambao ulifanyika juzi katika ofisi za timu hiyo Kilimani ulisimamiwa na Makamo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Zanzibar ZFA wilaya ya Mjini  Juma Abdurabi ambae ndie aliekuwa Mwenyekiti wa uchaguzi huo akisaidiwa na katibu wake Yahya Juma Ali. Mbali na Mwenyekiti kuchaguliwa Ussi lakini pia wajumbe wa mkutano huo walimchaguwa Makame Issa Jecha kuwa Makamo Mwenyekiti. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Abdurabi alisema kuwa nafasi ya katibu ilichukuliwa na Saleh Abass nafasi ambayo awali nilikuwa ikishikiliwa na Abrahman Karume. Abass kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo atasaidiwa kazi  na Mwinyi Abdalla ambae amechaguliwa kuwa katibu Msaidizi wa timu hiyo. Viongozi wengine  waliochaguliwa ni Shaame Ali Hamad Mshika Fefha, Salum Iddi Ali Msaidizi Mshika Fedha na wajumbe watatu ni Ali Mang'aa, Malil Sultan na Nasra Juma Mohammed. Uongozi huo mpya uliochag...

Vijana wa tumbatu walia na huduma za afya inayopatikana hapo.

Vijana wa tumbatu wanaiyomba serikali ya mapinduzi ya zanzibar iwafikiriea kuwawekea huduma za vipimo vya x_ray ili kuepusha kuenda umbali mrefu kufata huduma hiyo wakiongea na mwandishi wetu kisiwani hapo kwa kutaka majina yao yasiwekwe hadharani wamesema huduma za afya zinazotolewa katika kituo cha afya kilichopo tumbatu hakikidhi haja na hupelekea wakati mwengine kuifuta huduma hiyo kivunge. Wamesema kati ya huduma ambazo wanazipata hutoka kwa nurs hata daktari muda mwendine hukosekana kituoni hapo Pia wamewaomba wahisani kuweza kusaidia jamii hiyo ambayo inaishi kwenye kisiwa kutoka mkokotoni hadi kufika tumbatu ni wastani wa nusu saa kwa kutumia usafiri wa jahazi lenye mashine.

UMSHIRIKIANO BAINA YA KINA MAMA WENYEWE KWA WENYEWE NI NJIA YA MAENDELEO NA USHINDI MKWA

WANAWAKE WA CCM WILAYA YA KATI WAMETAKIWA KUENDELEA KUDUMISHA MASHIRIKIANO NA MAELEWANO KWA LENGO LA KUKILETEA MAFANIKIO CHAMA HICHO. KAULI HIYO IMETOLEWA KATIKA TAWI LA CCM TUNGUU NA DIWANI WA KUTEULIWA NDUGU SALUM KHAMIS KIBESHI WAKATI ALIPOKUWA AKIUFUNGUA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WANAWAKE U.W.T JIMBO LA TUNGUU. AMESEMA MASHIRIKIANO NA UMOJA KWA WANAWAKE WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDIO NJIA PEKEE ITAKAYOPELEKEA KUIMARIKA KWA CHAMA HICHO NA KUKIPATIA USHINDI MKUBWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020. AIDHA AMEWATAKA WALE AMBAO HAWAKUFANIKIWA KUPATA KURA ZA KUTOSHA KATIKA UCHAGUZI HUO KUACHANA NA MAKUNDI NA BADALA YAKE KUWA KITU KIMOJA NA KUTOA MASHIRIKIANO YA KUTOSHA KWA VIONGOZI WAPYA WALIOCHAGULIWA  ILI KUPELEKA MBELE MAENDELEO YA CHAMA HICHO. WAJUMBE WA MKUTANO HUO MKUU WAMEMCHAGUA NDUGU BAHATI ISSA SULEIMAN KUWA MWENYEKITI WA U.W.T JIMBO LA TUNGUU KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO.  AIDHA PIA WAMEWACHAGUA WAJUMBE 4 WA MKUTANO MKUU MKOA, WAJUMBE 2 MKUTANO MK...

WILAYA YA MJINI YAJIPANGA VYEMA KUANZA MASHINDANO YA MTOANO

MICHUANO ya ligi ya Mtoano inatarajiwa kuanza rasmi kesho  kwa kupigwa michezo  miwili itakayochezwa saa  8 na saa  10 za jioni. Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na ZFA wilaya ya mjini inashirikisha timu nane  za madaraja tofauti. Afisa Habari  wa chama hicho Mwajuma Juma ameliambia dayari la Michezo  kwamba timu 16 zitashiriki ligi hiyo na mchezo wa kwanza utachezwa saa  8:00 mchana kati ya Hawai na Urafiki. Aidha alisema kuwa mchezo  mwengine utachezwa saa  10:00 ambao utawakutanisha timu ya Shaba kutoka Pemba na African Coast. Alisema kuwa chama chao kimekuwa na kawaida ya kuandaa mashindano hayo kila mwaka kwa madhumuni ya kuzipa mazoezi timu ya kujiandaa na ligi.ab Aidha alizitaja timu nyengine zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Negro United, Gereji, New Kingi, Polisi Bridge, Mwembemakumbi, Raska Zone City, Kundemba, Elhilal, Black Sailor, Polisi, Ujamaa na Mwembeladu.