Posts

Image

LIGI KUU ZENJ YAKARIBIA KUMALIZIKA KUTAFUTA TIMU 8 BORA NA 12 ZAKUSHUKA DARAJA

LIGI KUU ZENJ YAKARIBIA KUMALIZIKA KUTAFUTA TIMU 8 BORA NA 12 ZAKUSHUKA DARAJA Mzunguko wa 33 wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja unatarajiwa kuanza rasmi kesho Ijumaa kwa kupigwa michezo mitatu katika Viwanja viwili tofauti Amaan na Fuoni. Ratiba ya mzunguko wa 33 ligi kuu ya soka Zanzibar kanda ya Unguja hiyo. Ijumaa 28/4 Kipanga vs KVZ saa 10:00 Fuoni. Ijumaa 28/4 KMKM vs Malindi saa 10:00 Amaan. Ijumaa 28/4 Taifa vs Chuoni saa 1:00 usiku Amaan. J/mosi 29/4 Polisi vs Kijichi saa 10:00 Fuoni J/pili 30/4 Mafunzo vs Miembeni saa 8:00 Amaan J/pili 30/4 JKU vs Mundu saa 10:00 Amaan J/nne 02/5 Chwaka vs Zimamoto saa 8:00 Amaan J/nne 02/5 B/Sailors vs Kimbunga saa 10:00 Amaan J/nne 02/5 Kilimani C vs J/Boys saa 1:00 usiku. Timu 2 kati ya nne zilizojihakikishia kutinga hatua ya 8 bora kutoka kanda ya Unguja ni kinara JKU yenye alama 69, Jang’ombe Boys alama 66 huku Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya tatu na Zimamoto inayokamana nafasi ya nne...

CITY KAMILI KUWAKABILI SEBLEN LEO, KAMBI YA MUDA MREFU YAWAPA KIBURI

Image
CITY KAMILI KUWAKABILI SEBLEN LEO.. Timu ya Miembeni City imemaliza mazoezi yake ya mwisho jana asubuhi ya kujiandaa na mchezo wao wa pili hatua ya nne bora ligi daraja la kwanza taifa Unguja dhidi ya Seblen mtanange ambao utavurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja. Miembeni City ambayo katika mchezo wake wa awali katika hatua hiyo ya nne bora iliibuka na ushindi wa magol 2-0 dhidi ya timu ya Charawe nakuendelea na maandalizi yake katika kambi ya timu hiyo iliyopo Dim ani wilaya ya magharibi B Unguja. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa timu hiyo Ali Khamis Ibny amesema ushindi katika mchezo wa awali dhidi ya Charawe uliamsha hamasa katika kambi yao na vijana wapo katika motisha ya hali ya juu yakufanya vyema katika kila mchezo uliopo mbele yao. Ibny Khamis amesema timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Miembeni wilaya ya mjini Unguja inaingia katika mchezo wa kesho na Seblen wakiwa na ari yakuibuka na ushindi huku maandalizi yao yakiwa yanarizisha kwa hali ya ju...

DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU

Image
NA BIN GHULLAM    DABI YA JANG'OMBE TAIFA HOI,WALIMWA KADI NYEKUNDU, WASHABIKI WAREMBEA CHUPA ZA MAJI UWANJANI mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa AMANI tarehe 25/4/2017 kati ya TAIFA YA JANGO'MBE wakombozi wa ng'ambu dhidi ya JANG'OMBE BOYS umemalizika kwa timu ya JANG'OMBE BOYS kushinda kwa goli moja kwa bila goli lililofongwa kwenye kipindi cha pili cha mchezo huo  mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna alieweza kuliona lango la mwenzake ikihesabika kwenye score boad 0-0 pia hata kadi moja ilikuwa bado haijatolewa licha ya mchezo huo kuchezwa kwa kukamiana pande zote mbili  Dakika chache tu kurudi katika mapumziko ndipo zikaanza kutolewa kadi ya kwanza ya njano kuoneshwa mchezaji  Andrian Mutu  na baadae kuja kuoneshwa ya pili na kufutiwa na kadi nyekundu.  Hadi mwisho wa mchezo BOYS 1 - 0 TAIFA ambapo mfungaji akiwa ni  KAMİS   MUSSA  (TRUMP) DKK 86 KAMİS   MUSSA  (TRUMP) mfungaji wa goli  Mchezo wa...

SAIDI MIRAJJI ABDALLA; "CUF JITAKARINI MURUDI MEZANI"

Image
MAKALA MAALUMU AMEIANDIKA SAIDI MIRAJI : TAFAKURI YA BABU. CUF MNAELEKEA WAPI JAMANI? Huko nyuma niliwahi kuandika makala fulani kuhusu mgogoro unaoendelea katika chama cha CUF na nikatanabahisha juu ya tabia ya kutukanana na kuanza kupigana wenyewe kwa wenyewe na athari zinazoweza kutokea. Bila ya kujali nani kafanya nini, baada ya tukio lililotokea leo la kushambuliwa waandishi wa habari, kupigwa watu kadhaa na wengine kujeruhiwa ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mali; KWA MTAZAMO WANGU sasa wakati umefika wa kufanyika yafuatayo:- Viongozi wa CUF na wanachama wake watafakari kwa kina madhara ya mbegu wanayoipanda kwa chama chao, katika jamii, katika tasnia ya siasa na hata kwa wao wenyewe binafsi kama mtu mmoja mmoja na familia zao. Viongozi wa juu wa CFU wanaoongoza pande zinazo kinzana wakemee kwa dhati tena hadharani tabia hizi ovu na kuwataka wafuasi wao kuwa watulivu wakati wakitafuta haki ya kila upande huko mahakamani, tena bila kushutumiana. Mahakama iharakishe ...
Image
baada ya haji manara kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya TFF makubwa yamemkuta HAJI SANDE MANARA.     Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba, Haji Manara. Pamoja na kufungiwa mwaka mmoja, Manara amepigwa faini ya Sh milioni 9. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu. Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara amefanya utovu mkubwa wa nidhamu kwa uwongozi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania na viongozi wake na ili kulinda heshma ya shirikisho hilo ndio wakapitia kwa kina matamshi aliyoyatoa manara na kubaini utovu wa nidhamu huo.

NA MWANDISHI WETU BIN GHULLAM.

UMOJA WA WATU WA TANGA ZANZIBAR WAZINDUA TIMU "TANGA CITY" umoja wa watu wa tanga visiwani zanzibar umezindua timu yao ambayo wameipa jina la TANGA CITY akiongea katika ghafla hiyo mgeni rasmi ambae ni mwenyekiti wa ZFA wilaya ya mjini ndugu HASSAN HAJJI HAMZA almaarufu COACH CHURA amewataka kutunza nidhamu na kuacha kutegemea wanasiasa katika kuendeleza shughuli zao za michezo.   Katika nasaha zake hizo mwenyekiti wa FA MJINI CHURA amesema wakipewa chochote kutoka kwa mtu yoyote wapokee na wasiache ila waondoe tegemeo kutoka kwa wabunge na wawakilishi, jengine aliloliasa CHURA ni viongozi kujuwa wajibu wao na kuwa wastahamilivu wakati wa kusimamia majukumu yao kwa vile wanaweza kukutana na maonevu ya bahati mbaya au ya makusudi .   Timu ya TANGA CITY imeanzishwa miezi nane iliyopita na kujipima nguvu na timu za madaraja kadhaa na kuweza kuzifunga hapo ndio walipoona ipo haja kuisajili timu hiyo kwenye chama cha mpira wa miguu wilaya ya mjini   Akisoma risala ya timu ...