CITY KAMILI KUWAKABILI SEBLEN LEO, KAMBI YA MUDA MREFU YAWAPA KIBURI
CITY KAMILI KUWAKABILI SEBLEN LEO..
Timu ya Miembeni City imemaliza mazoezi yake ya mwisho jana asubuhi ya kujiandaa na mchezo wao wa pili hatua ya nne bora ligi daraja la kwanza taifa Unguja dhidi ya Seblen mtanange ambao utavurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja.
Miembeni City ambayo katika mchezo wake wa awali katika hatua hiyo ya nne bora iliibuka na ushindi wa magol 2-0 dhidi ya timu ya Charawe nakuendelea na maandalizi yake katika kambi ya timu hiyo iliyopo Dimani wilaya ya magharibi B Unguja.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa timu hiyo Ali Khamis Ibny amesema ushindi katika mchezo wa awali dhidi ya Charawe uliamsha hamasa katika kambi yao na vijana wapo katika motisha ya hali ya juu yakufanya vyema katika kila mchezo uliopo mbele yao.
Ibny Khamis amesema timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Miembeni wilaya ya mjini Unguja inaingia katika mchezo wa kesho na Seblen wakiwa na ari yakuibuka na ushindi huku maandalizi yao yakiwa yanarizisha kwa hali ya juu.
Kuhusu majeruhi mkuu wa kitengo cha habari wa timu hiyo amesema hakuna mchezaji hata mmoja ambae yupo majeruhi na nyota wote waliopo kambini wamefanya mazoezi ya mwisho asubuhi ya leo huku hamasa na ari ya mchezo wa kesho na Seblen ikiwa imeongezeka maradufu.
Miembeni City ambayo katika mchezo wake wa mwanzo wa hatua hiyo ya nne bora iliibuka na ushindi wa magol 2-0 dhidi ya Charawe yaliyofungwa na Muhamed Vuai (Prince) na Seif Salum (Zola) ushindi wa kesho dhidi ya Seblen unaifanya timu hiyo kujikatia tiketi yakushiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu wa 2017-2018.
Miembeni City inaingia katika mchezo huo wakiwa wanalingana kwa pointi na Ngome ya Fuoni ambayo nayo iliibuka na ushindi katika mchezo wa awali na timu ya Seblen kwa kuwafunga magol 2-1.
Michezo ya hatua ya nne bora itakayopigwa leo katika dimba la Amani Miembeni city anacheza na Seblen mnamo majira ya saa kumi alasiri huku Charawe akicheza na Seblen mnamo majira ya saa moja usiku.
Comments
Post a Comment