Posts

Showing posts from September, 2024

Mshike mshike wa Polisi Jamii Cup magharibi B

Image
MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP WILAYA MAGHARIBI B YALIENDELEA TENA KWENYE VIWANJA VIWILI TOFAUTI.KWENYE DIMBA LA  KIEMBE SAMAKI KULIKUWA NA PAMBANO KATI YA NYAMANZI CITY NA CHUNGA CITY MATOKEO IKIWA NI GOLI  4 KWA  1 MAGOLI YA CHUNGA YALIFUNGWA NA YASSIR MOHD DAKIKA YA 7 NA GOLI LA PILI  LILIFUNGWA TENA NA YASSIR MOHD DAKIKA YA 12. NA BAO LA KUFUTIA MACHOZI LA NYAMANZI CITY LIMEFUNGWA DAKIKA YA 39 NYAMANZI WALIPATA BAO LA KUFUTIA MACHOZI LILILOFUNGWA NA JUMA KOTO .DAKIKA YA 68 SAID SALUM ALIPATIA TENA CHUNGA CITY BAO LA TATU NA DAKIKA YA78 EVEREST ALIPATIA CHUNGA CITY GOLI LA NNE. KWENYE MCHEZO HUO  MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP NA MKUU WA KITUO CHA POLISI MAZIZINI SP- SALUM NGAYANA ALIMKABIDHI MPIRA YASSIR MOHD KWA KUWA MAN OF THE MATCH ALIPATIA MABAO MAWILI NA ASSIST MBILI . KULE DIMBA LA NGOME KULIKUWA NA MPAMBANO KATI YA SHUBA SHUBA FC NA KOMBENI FC MATOKEO NI KOMBENI FC WAMESHINDA KWA PENATI 5 KWA 4 DHIDI YA SHUBA SHU...

KMKM yaondoka na alama tatu kibindoni kio

Image
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo kocha msaidizi wa Ibrahim Khamis Khatib amesema wapinzani wao walikuja kwa kupania mchezo ndio kilichowafanya washinde magoli wawili. Amesema mchazaji samir ametoka kwenye majeraha ndio maana hayukp vizuri. Ibrahim amewataka washabiki wa KMKM kuja viwanjani kuona kandanda inavyochezwa. Nae kocha wa muembe makumbi Rajab Mrisho amesema waamuzi bado wana mapungufu ndio maana wamepoteza mchezo wa leo. Amesema mchezo ulianza vizuri kipindi cha kwanza mabadiliko yamekuja kipindi cha pili amedai licha ya mchezo kwenda nao vizuri, wachezaji wake wamejituma wakishindwa kwenye mipango na kupelekea kufungwa goli mbili kwa moja.

Historia ya Majestic cinema.

Image
Historia Ya Majestic Cinema Na  Kuunguwa  Moto. Majestic Cinema, iliyofunguliwa mnamo Oktoba 20, 1955, baada ya jengo la kwanza la sinema kuunguwa, ilikuwa ni fahari ya Zanzibar, Ilibuniwa na mbunifu maarufu  Mzanzibari Dayalji Pitamber Sachania, baada ya sinema ya awali, Royal Cinema iliyojengwa 1921, kuteketea kwa moto mnamo Februari 8, 1954 ,siku hiyo kulikuwa na Zanana show ,ingawa nje kulikuwa na mabarobaro tele wakitia macho nuru, siku ambayo ikiendeshwa filamu inayoitwa Albela.Albela ni filamu ya vichekesho na  muziki ya Bollywood ya 1951 iliyoongozwa na nyota Bhagwan Dada na Geeta Bali. Sinema  Yakihindi ilikuwa ya  kwanza kwa  mapato ya juu kwa wakati huo na sinema ilijaa wanawake ikaleta mtafaruku mkubwa  . Royal Cinema, iliyokuwa sinema ya kwanza ya kifahari katika Afrika Mashariki, ilifunguliwa na Hassanali Adamjee Jariwalla na kubuniwa na J.H. Sinclair,  Majestic Cinema ilikuwa na muundo  mpya wa kipekee wa vishubaka vya mis...

Photo from Ali Ghullam

Image
Petroleum imepanda kwa shilling mia moja na mbili kwa bei mpya ya mwezi wa tisa, ambapo bei ya awali ilikua ni 3063 , wakati bei ya diesel imeshuka kwa shilling kumi na mbili ambapo awali ilikua ikiuzwa kwa shilling 3259 na bei ya mafuta ya taa ikibaki kawa ilivyo haikuongezeka wala kupanda. Bei ya mafuta ya ndege yakushuka kwa shillings sita ambapo yalikuwa yakiuzwa kwa shs 2843. Hii imetokana na taarifa zinazo tolewa na mamlaka ya maji na nishati Zanzibar ZURA leo tarehe 8 September 2024 huko ofisini kwao maisara mjini Unguja.

KUELEKEA MCHEZO WA MUEMBE MAKUMBI NA NEW CITY TAMBO HIZI APA.

Image