MPENDAE KUFYEKA BUSTANI ZILIZOKOSA HUDUMA NA MBOGAMBOGA ZAKE.
WANANACHI WA WADI YA MPENDAE WAMESHAURIWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUWEKA MAZINGIRA SAFI YA WADI HIYO ILI KUJIEPUSHA NA MARADHI YA MRIPUKO.
AKIZUNGUMZA KATIKA MUENDELEZO WA ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIMBO LA MPENDAE DIWANI WA WADI HIYO SHARIFA MUHAMMED AMESEMA LENGO LA ZOEZI HILO NI KUHAKIKISHA MAENEO YA JIMBO HILO YANAKUWA KATIKA HALI YA USAFI WAKATI WOTE.
AKIWAZUNGUMZIA WANANCHI AMBAO HAWASHIRIKI KATIKA ZOEZI HILO LINALOFIKA KATIKA MAENEO HAYO DIWANI SHARIFA AMESEMA WAMEWEKA SHERIA NDOGONDOGO YA KUWATOZA FAINI WANANCHI HAO.
SHEHA WA SHEHIA YA MPENDAE SULEIMAN ALI MAKUU AMEFAHAMISHA KUWA ZOEZI HILO NI ENDELEVU AMBALO WANANCHI WANAPASWA KUSHIRIKIA ILI KUWEKA MAZINGIRA SAFI YA MAENEO YAO.
KWA UPANDE WAO BAADHI YA WANANCHI WALIOSHIRIKIA KATIKA ZOEZI HILO WAMEWASISITIZA WANANCHI WEZAO KUSHIRIKIANA KATIKA KUYALINDA NA KUYATUNZA MAZINGIRA YA MAENEO HAYO.
ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIMBO LA MPENDAE NI ENDELEVU AMBALO KUFANYIKA MWANZO WA MWEZI NA MWISHI WA MWEZI KWA LENGO LA KUWEKA MAZINGIRA SAFI NA JIMBO HILO.
Comments
Post a Comment