MICHEZO MIDOGO INAANZA KUIMARISHWA KUPITIA SHAMRASHAMRA ZA SHEREHE ZA MAPINDUZI
Mchezaji Makame Juma (Ronaldo) amefanikiwa kushinda kombe la Draft Mapinduzi Cup baada ya kumfunga Azizi Abdallah (Ostadh) kwa mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Maskani ya Stone Baret iliyopo Kibanda Maiti. Akiyafunga Mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana amesema lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuinua michezo yote ili vijana wapate fursa mbali mbali kupitia michezo. Nae Mbunge wa Jimbo Shaurimoyo Mattar Ali Salum ambae nae alishiriki Katika Mashindano hayo, amesema msimu ujao wanatarajia kuyaboresha Mashindano hayo kwa kushirikisha wachezaji wengi kutoka majimbo tofauti huku mshindi akitarajiwa kupewa zawadi ya Mbuzi Mnyama. Mchezaji Aziz Abdallah ambae ameshindwa kwenye fainali amezungumza na ZBC huku akisesema Mashindano hayo yalikuwa na ushindani mkubwa ambapo amekiri mpinzani wake alimzidi kiwango. Bingwa wa Mashindano hayo Makame Juma (Ronaldo) amesema alijiandaa...