Posts

Michezo inawajenga kiakili wanafunzi na wazee wao.

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Tabia Maulid Mwita, amewataka walimu na wazazi kushirikiana katika kukuza na kulea vipaji vya wanafunzi. Hayo ameyaeleza wakati akifunga   Tamasha la tatu la Michezo la Skuli ya Leera la mwaka 2024 lililofanyika  kwenye uwanja wa Amani Complex . Alisema watoto hao watakapoekewa mashirikiano baina pande zone mbili watakuja peperusha bendera ya Taifa katika kuimarisha michezo. Aliwataka skuli ya Leera kuendelea kuibua vipaji kwani miundo mbinu ya michezo inaendelea kukua kwa kasi zaidi pia ni vyema kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa jitihada za kuimarisha sekta ya Michezo nchini. Waziri Tabia alieleza Serikali imetenga fedha billion 70 katika sekta ya michezo, hivyo hawanabudi kuthamini michezo na kuiendeleza katika skuli kwa watoto wao. Akisoma risala ya Skuli hiyo  Mkuu  wa  Utawala Jonathan Kahatano, alisema skuli hiyo inatoa taaluma bora ikiambatana ...

ALMUBARAK na ZOI wakubali kuwa madaraja ya fainali.

Image
Baada ya kukubali kipigo cha goli moja bila chuo cha Almubarak almazruwi kutoka kwa Mafundi umeme wa magomeni makada chuo cha Microtech kesho wata ,  jitupa uwanjani kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya watembeza watalii wa Amani ZOI language waliofanywa daraja na chuo cha Microtech kwa kutandikwa bakora mbili bila majibu. Kesho asubuhi ZOI na Almubarak watacheza kujua nafasi ya tatu na ya nne. Mchezo wa fainali utapigwa Mao ze Dong siku ya Jumapili hii ikiwakutanisha ICPS wakiumana na Microtech.

WALIWOONGOZA KWENYE MAKUNDI WAKWAMA KWA NAMBA NNE.

Image
Mashindano ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo na vituo vya mafunzo ya amali yameingia hatua ya nusu fainali baada ya kukamilisha hatua ya robo leo asubuhi kuchezwa michezo minne mapema asubuhi ilipigwa mbungi kali kati ya walima michicha wa JKU dhidi ya wafanya biashara wa chukwani ICPS , ambapo dakika 90 za uwanjani walimaliza kwa sare ya goli moja kwa moja na kwenda hatua ya changamoto ya mikwaju ya penalty ambapo JKU wakipoteza mikwaju miwili na ICPS wakiweka kambani yote. Mchezo mwengine ikuwa kati ya maustadhi wa Almubarak almazruwi waliokuwa na kibarua kizito kwa wafanya biashara wa kisima majongoo Zanzibar Commercial, hiyo ikiwa ni kwa michezo ya saa mbili. Michezo ya saa nne izikutanisha Microtech waliopata ushindi rahisi mbele ya warembo wa miembeni Green Woman wa magoli matatu bila, huku waandaaji wa vyakula na vinywaji Mkokotoni wakikaribishwa kwenye vivutio vya utalii na watembeza watalii wa Amani ZOI kwa misumari miwili ya jahazi bila majibu. Kesho ligi hiyo itaendelea...

Makunduchi, INCLUSIVE,za bwagwa robo fainali mashindano ya VTA.

Image
Baada ya kukamilisha hatua ya makundi ligi ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali leo timu nane 8 zatinga robo fainali ZOI language ikikamilisha idadi hiyo baada ya ushindi wa goli mbili bila dhidi ya watafsiri maneno kwenda ishara chuo cha Inclusive kwenye mchezo wa kiporo kilicho wanufaisha ZOI. Timu ya Makunduchi, Inclusive na Mwanakwerekwe zikimaliza hatua ya makundi kwenye kundi A. Na upande wa kundi B chuo cha ZAWA, DHOW Country na chuo cha Mwenge wote wakiishia safari yao hapo wakiwaavha mafahali waendelee na vita hapo kesho katika hatua ya robo fainali. Vyuo hivyo ni Zanzibar Commercial atakipiga dhidi ya Almubarak, JKU atapigishana kwata na ICPS, ZOI wakijaribu bahati yao kwa wahudumu wa hotelini Mkokotoni, huku Microtech wanawsalika warembo wa miembeni Green Woman.

JKU YAMALIZA MAKUNDI KWA KUWEKA HESHMA.

Image
Timu ya chuo cha ufundi JKU kimezima harakati za burudani kutoka mizingani forodhani kwa DHOW Country baada ya kuwaadabisha kwa bakora sita mtawalia katika mchezo wa mapema asubuhi ya leo. JKU walikuja kamili kuisaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi B ambapo katika kundi hilo yeye na Microtech ndio wanagombea nafasi hiyo. Wakati wapinzani wao DHOW Country walikuja pungufu na kuwafanya JKU wapate wepesi wa ushindi huo mkubwa. Michezo mengine ikiwakutnisha ZOI watembeza watalii wa Amani waliofungwa goli mbili kwa moja dhidi ya wafanya biashara wa kisima majongoo Zanzibar Commercial ambao bado wapo kileleni baada ya ushindi wa leo wakikusanya alama kumi na tatu 13 ambapo kwenye group lao hakuna atae fikisha. Chuo cha Almubarak almazruwi wakikubali kipigo cha goli moja kwa nunge dhidi ya Watoa huduma hotelini Mkokotoni, mchezo wa mwisho ikiwakutanisha ndugu wawili kati ya Mwanakwerekwe dhidi ya Makunduchi, ambapo wote wakiweka tegemeo la adui muombee njaa ili wapate nafasi ya kutin...

Microtech na Green Woman wakata tiketi ya Robo fainali.

Image
Baada ya kukamilisha michezo 6 sita ya kundi B chuo cha Microtech wamekata tiketi ya Robo fainali ya michuano ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali baada ya ushindi wa goli moja kwa nunge dhidi ya watoa huduma hotelini Mkokotoni na kuwasafirisha hadi nafasi ya kwanza wakisubiri hatma ya kubakia hapo baada ya mchezo wa mwisho wa JKU. Warembo wa miembeni Green Woman nao tayari wamekata tiketi hiyo ya robo fainali baada ya kukamilisha michezo 6 sita ya kundi A na kuondoka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya watafsiri maneno kutoka mombasasa Inclusive ambao bado wapo kwenye mabano kutinga robo fainali ya kundi hilo, timu nyengine iliyokamilisha michezo 6 sita ni ICPS wenye alama 9 tisa, Green Woman wameungana na Zanzibar Commercial wenye alama 10 licha ya kipigo cha leo kutoka kwa ICPS cha goli mbili bila. Michezo mengine ni Maustadhi wa Almubarak almazruwi wakiwaadhibu wapiga za music DHOW Country goli mbili bila majibu.

Microtech yaramba shubiri ya wakulima wa mpunga JKU.

Image
Baada ya ushindi wa michezo minne mfululizo Microtech hatimae leo ameonja chungu ya jiwe baada ya kupokea kipigo cha paka mwizi kutoka kwa wakulima wa mpunga JKU cha misumari minne kwa moja katika mchezo wa mapema ulikuwa wa kutafuta nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi lao. Mchezo mwengine uliwakutanisha wacheza kibati kutoka Amani mkoa na Mafundi magari kutoka Mkokotoni ambapo karata zao hazikutoa mbabe na badala yake kugawana alama moja kwa sare tasa ya sifuri bin sifuri. Michezo mengine ya saa nne ikiwakutnisha ZOI watembeza watalii wa Amani dhidi ya wafanya biashara wa chukwani ICPS kwa kutoka suluhu ya goli 2 mbili kwa mbili, mchezo uliochezwa kwa tahadhari kubwa kila upande  Mchezo wa mwisho ulionesha mpira kukosa huruma kwa jenenza la wavuvi wa tasi na pono wa Makunduchi kugongomelewa msumari wa moto na warembo wa miembeni Green Woman kwa kichapo cha goli moja kwa nunge. Mashindano hayo ya Elimu bila malipo kwa mkoa wa vyuo vya mafunzo ya amali yanaendelea tena kesho k...